MCHUNGAJI ATOROKA NA KAPU LA SADAKA.
Tukio la ajabu limetokea katika kijiji cha Misuu, Kaunti ya Machakos nchini Kenya baada ya pasta mgeni kutoroka na kapu lililokuwa limejaa sadaka wakati waumini walipokuwa wamefunga macho kwa ajili ya kufanya maombi.
Taarifa zinasema kuwa pasta wa kanisa hilo alimualika mwenzake kutoka kaunti jirani ili awalishe waumini chakula cha kiroho na hatimaye kuongoza harambee ya ujenzi wa kanisa hilo.
Kila mmoja alianza kuomba kwa ndimi na kupandwa na jazba kubwa! Ni wakati huo pasta mgeni alipotoroka na kikapu cha pesa:
“Mtumishi wa Mungu alikuwa na matumaini makubwa kuwa mwenzake angechangisha pesa nyingi katika harambee hiyo kwa sababu alikuwa na ufasaha wa kuongea. Hii ndio sababu kuu ya kumualika kanisani,” alisema mtoa taarifa.
Katika ripoti hiyo ya Jumanne, Februari 19 ambayo TUKO.co.ke imeisoma, wakati wa ibada ulipowadia, kanisa lilikuwa limejaa.
Kwaya iliburudisha kwa nyimbo mbili kisha pasta akanyanyuka na kumkaribisha mgeni.
Inaelezwa kuwa bado pasta wa kanisa hilo anamsaka mgeni wake ili amchukulie hatua za kisheria na kulazimishwa kurejesha pesa hizo.
“Wajua mahubiri ya pasta huyo mgeni yalikuwa moto moto na yaliwagusa wengi rohoni,” anasema mtoa taarifa.
Inadaiwa kwamba, sadaka zilitolewa kwa wingi na kikapu kikawekwa madhabahuni alipokuwa ameketi pasta huyo mgeni.
Baada ya kipindi cha mahubiri, inadaiwa kwamba pasta wa kanisa hilo aliinuka na akawaongoza waumini kwa maombi kabla ya kuanza mchango.
Duru za mtaani zanasema kuwa, waumini walipomaliza maombi na kufungua macho yao, walipigwa na butwaa walipopata mgeni wao hayupo na mfuko wa sadaka ulikuwa hauonekani.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, juhudi za waumini kumsaka pasta huyo ziliambulia patupu maana alikuwa ametokomea na kila alipopigiwa simu jibu lilikuwa, “Mteja wa nambari uliyopiga hapatikani kwa sasa.”
Waumini na pasta wao waliishia kuduwaa huku wakimlaani kwa kuiba sadaka bila kuhofia adhabu kali ya Mungu.
Post a Comment