Polisi Dodoma yawatia mabaroni Watuhumiwa wizi wa hati za viwanja

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linawashikilia watuhumiwa wanne kwa makosa ya wizi wa hati za viwanja, kubadili ramani za mpango mji na kuuza viwanja kwa njia ya utapeli.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Gilles
Muroto amesema watu wamekuwa wakipelekea migogoro ya ardhi kwa wananchi
kutokana na tabia hiyo.
"Wanasababisha
migogoro mingi ya ardhi katika Jiji letu la Dodoma, wanashirikiana na
watumishi ambao sio waaminifu na kupelekea kuingilia mifumo ya
halmashauri ya ardhi," amesema.
Amesema
kuwa watuhumiwa wote wanahojiwa kuhusiana na kugushi nyaraka za ardhi
na wamepekuliwa na nyaraka wamekutwa nazo na muda wowote watafikishwa
mahakamani pindi uchunguzi uatakapokamilika.
Post a Comment