Ads

WATUHUMIWA MAUAJI YA WATOTO MKOANI NJOMBE WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Watuhumiwa watatu wa matukio ya mauaji ya watoto mkoani Njombe Leo Jumanne February 12, 2019 wamefikishwa mahakamani katika mahakama ya hakimu mkazi Njombe akiwemo Joel Nziku  ambaye ni mtuhumiwa wa mauaji ya watoto watatu wa familia moja ya Danford Nziku mkazi wa Ikando halmashauri ya wilaya ya Njombe.

Watuhumiwa wengine ni Nasson  Kaduma na Alphonce Danda. 

Nje ya mahakama hiyo ulinzi umeimarishwa kutokana na polisi kusambaa kila kona, huku msafara wa watuhumiwa hao ukisindikizwa na magari sita ya polisi.

No comments