DC KIGAMBONI AELEZA SABABU YA KUCHELEWA KUKAMILIKA UJENZI KITUO CHA AFYA KIMBIJI.
Mkuu wa
Wilaya ya Kigamboni Mhe.Sarah Msafiri , ameishukuru kamati ya Ujenzi Manispaaya Kigamboni kwa
kusimamia vizuri hadi kukamilika ujenzi
wa kituo cha Afya Kimbiji huku akiishukuruserikali
kuu kwa kutoa fedha kwaajili ya ujenzi huo ambao umegharimu jumla
ya shilingi million 450.
DC Msafiri
ametoa pongezi hizo leo wakati wa ziarayake ya kukagua miradi ya ujenzi Wilayani humo ambapo ameeleza sababu za kuchewa kukamilika
kwa ujenzi huo kuwa ni pamoja na
jiografia ya eneo na kuongezeka kwa wingi wa vyumba vya Majengo .
‘’Majengo ya
kituo chetu nitofauti na mengine nchini ambayo tulipewa wote fedha za kuanza
ujenzi eneo hili lina mwinuko (Land scape) ilituchukua muda kuweka sawana na
kuanza ujenzi wa msingi ,pia sisi tumeongeza vyuma sita kwahiyo tukachelewa kumaliza ila kwasasa
asilimia 90% ya ujenzi imekamilika”Alisema .
Aidha
amesema pamoja na kukamilika kwa ujenzi huo wanatarajia kupokea vifaatiba
kutoka kwa MSD ifikapo mwezi March na kuwataka wananchi wa maeneo jirani
kukitumia kituo hicho kwa kuwa serikali imewarahishia na kuwapunguzia usumbufu wa kutembea mwendo
mrefu kwenda vijibweni na Kigamboni kufuata huduma za Afya.
“Nawataka
sasa wananchi mkitumie kituo hiki kata
zote nne zinazo zunguka eneo hili tumieni hiki ni kituochenu ,naomba pia
uongozi wa kituo hiki pia muwatangazie wananchi ili wasiendelee kupata
shida”Alisema
Kwa upende
wake Mganga mkuu wa Manispaa ya Kigamboni , Charles Rashid Mkombachepa, baadhi ya huduma zimesha
anza kutolewa ikiwemo huduma ya Mama na Mtoto na .
“Kituo hiki
tangu tungu tumekifungua mwezi mmoja uliopita jumla ya akina mama 25 wamesha
jigulia hapa naendelea kutoa wito kwa wananchi waje kupata huma hapa”Alisema
Katika
ujenzi huo jumla ya shilingi million
450, ambapo serikali kuu imetoa shilingi million 400 ambapo kutoka na
jiogafia ya eneo hilo na kuonezeka idadi ya vyumba gharama zilidi ambapo
Manispaa ya kigamboni iliongezea shilingi milino 50.
Post a Comment