Balozi Seif Ali Iddi kufungua Mashindano ya Michezo ya Majeshi Jumamosi
Hussein
Ndubikile
Mwamba wa
habari
Makamu
wa
Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Ufunguzi wa Mashindano ya Michezo ya Majeshi yatakayoanza kuanzia
Februari 23 hadi Machi 8 mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Hayo
yamesemwa leo jijini humo na Menyekiti wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania
(BAMMATA) Brigedia Jenerali, Suleiman Mzee ambapo amesema michezo hiyo
itashirikisha vikosi kutoka kanda saba za majeshi likiwemo Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ), Jeshi la Uhamiaji, Jeshi la Polisi nchini, Magereza, Jeshi la
Kujenga Taifa(JKT) na Zimamoto na Uokoaji.
“ Mashindano
hufanyika kila mwaka tumewaalika wageni wa heshima tunatarajia Balozi Seif Ali
Idd kutufungulia mashindano Uwanja wa Uhuru,” amesema Brigedia Jenerali Mzee.
Amebainisha
kuwa mashindano hayo yatashirikisha michezo mbalimbali ikiwemo ya mpira wa
pete, mpira wa miguu, mpira mikono wanawake na wanaume, Ndondi, mpira wa wavu,
kikapu, kulenga shabaha wanawake na wanaume pamoja na riadha.
Amesisitiza
kuwa michezo hiyo itafungwa na Waziri wa Ulinzi, Dkt. Hussein Mwinyi na kwamba
lengo la mashindano ni kuendeleza elimu ya viungo na utimamu ndani ya jeshi,
kuinua vipaji vya kwa wanamichezo pamoja na kuandaa mashindano ya ulinzi na
uslalama.
Amefafanua
kuwa baada ya Waziri Dkt. Mwinyi jioni kutakuwa na hafla ambapo Waziri wa Habari,
Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.
Brigedia
Jenerali Mzee amesema Kauli mbiu ya michezo hiyo kwa mwaka inasema Michezo ni
kazi na mshikamano na kuwaomba wananchi wa Dar na mikoa ya jirani kujitokeza
kwa wingi kushuhudia mashindano hayo.
Post a Comment