WAZIRI MKUU ACHUKIZWA NA TAARIFA YA KUZUIWA KWA NGUZO ZA UMEME
Aitisha kikao na viongozi wa maeneo hayo pamoja na Mawaziri husika
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amemuita
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happi pamoja na Wakuu wa Wilaya na
Wakurugenzi wa Halmashauri zote zinazozalisha nguzo za umeme katika mkoa
huo kufika ofisini kwake ili waeleze sababu za kuzuia nguzo za hizo
zisitoke.
“Wanieleze
kwa nini wanazuia nguzo,Wakati wananchi wanasubiri kuunganishiwa huduma
ya nishati ya umeme wao wanazuia nguzo wanasubiri posho, Wanaidai
Serikali wakati ni wao ni sehemu ya Serikali Tutakutana ofisini kwangu
Januari 7, saa tano kamili asubuhi.”
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Ijumaa, Januari 4, 2019) wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji Nyoni, wilayani Mbinga akiwa katika siku ya tatu za ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma. Alisema jambo hilo linakwamisha zoezi la usambazaji umeme.
Aliyasema
hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi ambao
walilalamikia kitendo cha kutofikishiwa huduma ya umeme katika maeneo
yao kutokana na kukosekana kwa nguzo ambazo zimezuiwa kwa sababu ya
wahusika wanaidai Serikali posho.
Waziri
Mkuu alisema viongozi wengine watakaokuwepo kwenye kikao hicho ni
pamoja na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Waziri wa nchi
OR-TAMISEMI, Selemani Jafo,
Wenyeviti wa halmashauri hizo zilizozuia nguzo ili wamueleze sababu za kuzuia nguzo hizo.
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli iAlisema
Serikali imedhamiria kusambaza huduma ya nishati ya umeme katika vijiji
vyote nchini vikiwemo na wananchi hao wataunganishiwa umeme huo kwa
gharama ya sh. 27,000 tu.
Pia
Serikali imeondoa gharama za kulipia nguzo wala fomu za maombi ya
kuunganishiwa umeme, kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na
Serikali na kwa vijiji ambavyo viko kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi
vitafungiwa sola, jambo ambalo linalenga kufungua fursa za ajira na
kukuza uchumi kwa wananchi na Taifa.
Serikali
imefanya maamuzi hayo kwa sababu huduma hiyo ya umeme ni muhimu kwani
mbali ya kutumika katika matumizi ya majumbani, pia kwa kusogezwa karibu
na maeneo ya pembezoni itawezesha zahanati, shule ,viwanda na vituo vya
afya kuwa na umeme.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, JANUARI 5, 2019.
Post a Comment