WADAU WAFICHUA MBINU ZA UTOROSHAJI MADINI KUPITIA MATIKITI MAJI
Wadau wa madini wameeeleza jinsi madini nchini yanavyotoroshwa kwenda nje ya nchi kupitia mipakani.
Wadau hao wameeleza hayo leo Jumanne Januari 22, kwenye Mkutano wa Kisekta wa Wizara ya Madini ulioshirikisha wadau mbalimbali wa madini, baada ya Rais John Magufuli kutoa nafasi kwa wadau hao kuelezea changamoto zinazowakabili.
Mmoja wa wadau wa madini kutoka mkoani Geita, amesema madini hayo hutoroshwa na watu kutoka nje ya nchi kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwamo kuficha kwenye matikiti maji.
“Mtu anaweza akaiba dhahabu na kuweka hata kwenye ‘side mirror’, tikiti maji, kabichi, au tairi la spea, kwenye tikiti maji na kabichi anakata anaingiza kilo nyingi tu za dhahabu.
“Tukipata nafasi ya kuzungumza kwa utaratibu tutayasema haya yote, serikali inatoa taarifa ambazo sio sahihi ndiyo maana uliposema tujadili watu walipiga makofi.
“Pale Uwanja wa Ndege wa Mwanza, zile mashine ukienda na karatasi za namna fulani ukafunga madini unapita bila usumbufu wowote, nilienda kwenye kamati na tukakubaliana kwenda kuhakikisha na tulipofika ni sehemu moja tu ilionyesha kuna madini lakini sehemu nyingine hazikuonyesha,” amesema.
Mchimbaji
huyo mdogo wa almasi, amesema utoroshwaji madini unachangiwa kwa kiasi
kikubwa na wanunuzi wa ndani kunashindwa kumudu ukubwa wa ada za leseni
ambazo huhitaji zaidi ya Sh5 milioni.
“Tulikuwa
tunaomba kwa sisi kama wazawa angalau iwe Sh2 milioni, kwa wageni hata
ikiwekwa Dola 5,000 za Marekani haina shida,” amesema.
Mjumbe
wa Melema tawi la Mirerani, Fatuma Kikuyu amesema vijana walio nje ya
ukuta ni wengi kuliko waliopo ndani kutokana na kukosa mikataba na
kulipa mishahara.
“Ungetuachia
lile geti la Magufuli wazi ili vijana waingie kwenda kufanya kazi ili
kuopngeza pato la taifa, jambo ambalo linawasababisha kuruka ukuta hivyo
tunaomba tufanye kazi kama zamani,” amesema Fatuma.
Post a Comment