SOMA USHAURI ALIOTOA ASKOFU GWAJIMNA KWA RAIS MAGUFULI KUHUSU MADINI.
Mchungaji wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amemshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuunda timu ya watu wenye uzoefu mkubwa na wanaoijua siasa ya madini kimataifa, ili kuweza kupata soko kubwa zaidi.
Mch. Gwajima ametoa ushauri huo alipokuwa akizungumza mbele ya Rais Magufuli kwenye mkutano mkuu wa kisekta wa wizara ya madini.
Kwenye
ushauri huo Askofu Gwajima ambaye alianza kwa kumsifu Rais Magufuli,
amesema kwamba ni vyema akaunda timu ya watu wenye 'exposure' kwenye
siasa ya madini, kwani itasaidia kuweza kupenya kwenye soko la
kimataifa.
“
Leo umekuwa kama Nabii, nitoe ushauri kwa Mh. Rais, si kweli kama
hakuna soko la madini, dhahabu yenyewe ni fedha, isipokuwa nashauri kama
ikikupendeza, uwe na watu wenye exposure kwenye siasa za madini
kimataifa, sisi kwa asili tuna dhahabu, huwezi kutuambia tumechukua
dhahabu ya wengine tuthibitishe ni za kwetu, hizo ni siasa tu za masoko,
unaweza ukaunda watu wenye exposure ambao wanaweza kufikia masoko mbali
mbali duniani”, amesema Askofu Gwajima.
Sambamba
na hilo Mchungaji Gwajima ameendelea kueleza kwamba madini tuliyonayo
ni mengi na yanakosa soko kutokana na sababu mbali mbali, na iwapo
yangelipiwa ushuru yasingezagaa, hivyo kama ambavyo aliwahi kukutana
nayo watu wakiyauza kwenye bakuli barabarani.
"Nilipita
Mwadui nikashangaa, wakaniuliza tukuletee almasi kwa utani, ndani ya
saa moja watu walileta almasi imejaa bakuli haina watu wa kununua,
wametoka nazo ndani ya nyumba zao, hizo kama zingelipiwa ushuru nchi
yetu ingekuwa mahali pazuri sana”, amesema Gwajima
Hii
leo Rais Magufuli amefanya Mkutano na wadau wa Sekta ya Madini, ambao
pia uliwakutanisha na wadau na wafanyabiashara ya madini yaliyopo
nchini.
Post a Comment