MWENYEKITI UWT ILALA: UKIDONDOKA KIBIASHARA USIKATE TAAMAA ONAHAWA.
Na John Luhende
Mwamba wa habari
Mwenyekiti wa umoja wa
wanawake CCM (UWT) Wilayani Ilala, Amina Dodi ,amewataka wanawake
Wilayani Ilala kutokata tamaa katika ujasiliamali kutokana na changamoto
wanazo pitia bali ziwaimarishe kwa kuwaongezea uzoefu nakufikiri zaidi
kuzikifursa za kiuchumi.
Dodi , ametoa usahauri huo katika
semina ya Ujasiliamali ya kufunga mwaka 2018 na kuukaribisha mwakampya
2019 , ambapo amesema kuwa umoja
huo upo imara na umeendelea kupata wanachama wapya kila siku
kutokana na kazi nzuri zinazo fanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na kusema kuwa wanawake wa Ilala
wataendelea kumuunga mkono kwa kufanya kazi .
“Ninyi akina Mama mnafikilia kupatatu ,(kuwini ) maisha nipamoja na kupata elimu,
naomba niwatake tuwe watu wa wasomaji wa
habari mbalimbali ,hata Trump wa
Marekani ,alidondoka kibiashara akaja akainuka baadaye ,tuangalie Reginard
Mengi alikuwa na Gazeti Alasiri
akadondoka lakini hakukata tama,na kwenye uujasiliamali hutakiwi kukata tama wala
usije ukalalamika sana kwamba mimi mbona nafanya kazi nadondoka uwe makini tu nabiasharayako ukidondoka
utanyanukatu naomba wamama niwatie nguvu
mwaka huu 2019 utakuwa na mafanikio”Alisema.
Amesema ,mwaka uliopita ulikuwa na
mafanikio mengi kwa upande wa (UWT ) Ilala
na kwamba wameweza kutimiza malengo yao mengi ikiwemo kupata hati ya kiwanja chao ambacho wanakitafutia wawekezaji ili kuongeza kipato
cha umoja,na pia wameweza kuimarisha chama na umoja ,na wamepata semina
zakutosha kuhusu ujasiliamali na sasa wanaweza kuendesha siasana uchumi.
“Uchumi na saiasa vinakwenda sawa
wanawake hawa tumewajengea uwezo wa kujiimarisha kiuchumi na wanaweza kufanya
siasa safi ,unaweza kuwa na siasa lakini uchumi ukilegalega huwezi kufanikiwa,
kwahiyo kwaniaba ya wanawake (UWT ) Ilala tunamshukuru Rais kwa kujenga uchumi
na tunamuombea Mungu ampe Afyanjema iliaweze
kutekeleza mambo mengine mwaka huu 2019.
Katika semina hiyo wanawake hao
wamefundishwa mambo mbalimbali ikiwemo elimu juu ya Mikopo, namna
ya kuandika katiba ya vikundi ,na namna ya kubuni na kuanzisha biashara,Asha
Johari ni katibu UWT kata ya Gerezani yeye ameishukuru UWT ,Manispaa ya
Ilala na serikali kwa kutoa mikopo isiyo
na riba ambayo imekuwa ukombozi kwa akinamama ukilinganisha na miaka iliyopita
ambapo wanawake waliteseka kwa kutozwa riba kubwa.
“Tulikuwa tunapata mikopo kutoka kwa
mabenk ambayo ilikuwa nariba kubwa ya
asilimia kumi hadi kumi natano ya mkopo
sasa tunafaidika na huu usio na riba na tunajivuni serikalli hii inayoongozwa
na Chama Cha Mapinduzi, imemwokoa mwanamke kwa kiasi kikubwa “Alisema
Moja ya mambo ambayo yamerudisha nyuma
vikundi vingi nikuwa na katiba zisizo faa ,ambapo katika semina hiyo
yametolewa mafunzo ya kuandika katiba ,Ktiba ni muhimu sana na kilakikundi
kinahitaji Katiba kutokana na kutokuwa na ujuzi huu wa kuandika katiba vikundi
vingi vimekwama kupewa mikopo kutokana na kukopi Ktiba za vikundi vingine .
“Kwamafunzo haya majukumu yetu sasa kama viongozi ni kwenda
chini kwa kuwafundisha wanawake na hata
vijana ambao hawana mafunzo haya nao tuta wasaidia ii wapate katiba bora ‘’Alisema
Aziat Salim Juma Katibu UWT kata ya Buyuni.
Pamoja na hayo katika semina hiyo
wanawake wameweza kujifunza ni uthubutu
wa kuanzisha biashara , kujiamini na kuwa na mtazamo wa mbele zaidi kibiashara
na wamemshukuru Mwenyekiti kwa kuwapatia mkufunzi kutoka Uingereza ambaye pia
amewaahidi kuwa yatfutia masoko ya bidhaa zao .
“Ninachoweza kuwashauri wanawake
wajasiliamali wenzangu ni kuviweka
vituvyetu katika hali ya usafi zaidi viewe vya kisasa vinavyoweza kuuzika hadi
masoko ya nje nami nitashuka huko chini katika matawi kuwaelekeza ili waweze kuzingatia haya “ Alisema Magreth Cheka katibu UWT kata ya Kipawa.
Post a Comment