Ads

CCM TABATA Mtambani yatoa elimu kwa Jumuiya zake




Mwambawahabari
Katibu wa chama cha mapinduzi CCM tawi la TABATA Mtambani Ramadhani Kudunale akizunngumza katika moja ya mikutano ilioandaliwa na tawi la Mtambani.
Na Heri Shaban

CHAMA cha Mapinduzi CCM Tabata Mtambani yatoa Elimu kwa kuwapiga msasa Jumuiya za Chama hicho kwa kuwapa elimu kila kiongozi afahamu majukumu yake.

Semina hiyo iliandaliwa na CCM TABATA Mtambani ilifunguliwa DAR ES SAALAM Leo,na KATIBU wa CCM TABATA Haruna Aliphonce  ambapo katika ufunguzi alipiga marufuku TAARIFA za chama cha mapinduzi kujadiliwa mitandaoni badala yake aliwataka wana CCM masuala ya chama yasijadiliwe mitandaoni yafanyike katika vikao halali.

Haruna aliwataka wana CCM kutumia vikao vyao vya kanuni na kufuata taratibu za chama cha Mapinduzi waachane na utandawazi wa kutumia vikao vya chama kwa njia ya mitandao  .

Aidha alipongeza chama cha Mapinduzi MTAMBAN kwa hatua nzuri kutoa elimu ya kuwajengea uwezo Jumuiya za chama hicho kila Kiongozi kujua majujumu yake.

"Kila kiongozi wa CCM lazima awe na kazi halali ya kuwaingizia kipato,akielezea kazi ya Umoja wa VIJANA UVCCM ni walinzi wa chama kwa ajili ya kutafuta dora"alisema Haruna.

Pia alisema kazi kubwa ya Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT kuakikisha CCM ina shika dola na kuibuka kwa kishindo katika chaguzi zake.

  Aliwataka wana CCM kufuata kanuni za chama na kuwataka viongozi kulinda Siri za Chama cha Mapinduzi
Kwani kiongozi bora wa CCM atakiwi kutoa Siri za chama.

Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo hayo Katibu wa CCM mstaafu Charles Mabula alitoa mada kwa Jumuiya ya UWT,Wazazi,na UVCCM kwa kuwaeleza misingi yao na majukumu ya kila kiongozi.

Charles Mabula pia Katika mafunzo hayo ya CCM Mtambani aliwakumbusha makatibu wa CCM wote wawe wanatoa TAARIFA za vikao siku tatu kabla au wiki moja kabla, dhumuni ili kuwapata wajumbe wote katika kikao waache kutoa TAARIFA za kustukiza.

Katika mafunzo hayo Mabula aliwataka wana CCM kuacha tabia za Maneno ya uchochezi, Maneno machafu yasiofaa katika chama pia kiongozi kuchuja Maneno ndio sifa za wanachama au kiongozi bora.

Naye Katibu wa CCM TABATA Mtambani Ramadhani Kudunale aliwataka UWT, UVCCM, na Jumuiya ya WAZAZI, kuwahamasisha VIJANA katika kutoa elimu ya mikopo kwani siasa na UCHUMI.

Katibu Kudunale alizitaka jumuiya hizo kushirikiana Kuunda vikundi ili wachangamkie fursa za mikopo ya Serikali.

Alisema mafunzo hayo endelevu yatakuwa yanafanyika kwa Mwaka mara mbili dhumuni la Mafunzo hayo kuwakumbusha viongozi wa chama na Jumuiya kujua majukumu yao .


No comments