"Moto wa katibu mkuu CCM, Mimi Siufikii" RAIS DKT Magufuli.
Rais John Magufuli ameweka wazi kuwa hotuba za Katibu mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally huwa zinamshangaza kwa namna ambavyo anazitoa bila uoga jambo ambalo humfanya yeye ajione ni mpole.
Mwenyekiti
huyo wa CCM alieleza hilo jana kwenye hotuba yake wakati wa mapokezi ya
ndege ya pili aina ya Airbus A220-300 iliyowasili nchini jana mchana
Januari 11, 2019 kwenye Uwanja wa Ndege wa kimataifa Julius Nyerere
(JNIA) jijini Dar es Salaam.
''Dkt.
Bashiru amekuwa muwazi, huwa namuangalia kwenye hotuba zake saa
nyingine nasema kumbe mimi nafuu bwana kuliko huyu jamaa'', alisema.
Rais
alieleza kuwa Katibu wake huyo amekuwa akikemea ufisadi ambao ulikuwa
ukishamili siku hadi siku lakini sasa yeye anapingana nao hadharani bila
kujali.
Magufuli
amewataka viongozi wote wa chama na Serikali kuendelea kuwatumikia
wananchi kwa moyo mmoja ili kusaidia maendeleo na siku moja Tanzania
itakuwa kama Ulaya.
Post a Comment