ATCL YAPANGA SAFARI ZA DODOMA.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladislaus Matindi amesema kutokana na ongezeko la abiria, shirika hilo limeanzisha safari za kila siku kwenda Dodoma, kuanzia Januari 16, 2019.
Amesema hivi sasa ndege za shirika hilo zinafanya safari nne kwa siku kwenda Dodoma.
Ametoa
kauli hiyo jana Ijumaa Januari 11, 2019 katika hafla ya kupokea ndege
ya pili aina ya Airbus 220-300 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA).
Alisema
licha ya kuongeza safari hizo pia wanaendelea kufanya tathmini ya
uhitaji ili kuhakikisha Dodoma inaunganishwa na miji mingine ili
kurahisisha usafiri wake.
“Kuwasili
kwa ndege ni soko la kimkakati kusini mwa Afrika hususani nchi za
Zambia, Zimbabwe na Afrika Kusini lakini pia inaongeza uhakika wa kutoa
huduma katika maeneo yenye idadi kubwa ya watu ikiwemo Mwanza,
Kilimanjaro na Mbeya,” alisema Matindi.
“Hii
ni fursa muhimu katika kuhakikisha biashara yetu inakuwa endelevu na
tayari tumefanikiwa kuingia makubaliano usafirishaji wa nyama ya mbuzi
inayouzwa nje ya nchi kutoka Mwanza kuja Dar es Salaam kabla ya
kusafirishwa na mashirika mengine.”
Alisema
wanaendelea kushirikiana na shirika la ndege la Ethiopia na Misri ili
kuendeleza marubani na mpaka sasa wamefikia 50 kutoka 13 waliokuwepo
awali na hadi kufikia Aprili, 2019 watakuwa wamefikia 60 huku wahandisi
wakiwa 68 kutoka 15.
Amesema wahudumu wa ndege wamefikia 142 kutoka chini ya 20 walioanza nao na mpaka sasa wafanyakazi wa ATCL wanakaribia 300.
Post a Comment