JAMHURI YAIBANA AZAM FC KOMBE LA MAPINDUZI
Mabigwa watetezi wa kombe la Mapinduzi, Azam FC jana walianza kwa kupata sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Jamhuri katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar.
Kocha Mkuu wa Azam FC, Hans Pluijm amesema kwa sasa hesabu zao ni kwa mchezo wao unaofuata dhidi ya KVS utakaochezwa Januari 7 Uwanja wa Amaan.
"Tupo tayari kwa ajili ya michuano hii na tutafanya vizuri hasa kutokana na kikosi bora na wachezaji wenye uwezo wa kutafuta matokeo Uwanjani," alisema.
Michuano hiyo inatarajiwa kukamilika Januari 13 katika Uwanja wa Gombani,uliopo Pemba na mshindi atapewa zawadi ya shilingi Milioni 15 pamoja na medali.

Post a Comment