WAZIRI MKUU AFUNGUA KIWANJA CHA TAIFA CHA MCHEZO WA BASEBALL.
Mwambawahabari
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Kiwanja Kipya wa Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano ya Taifa ya Baseball kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Habari,
Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakati alipowasili
kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6,
2018 Kufungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua
Mashindano ya Taifa ya Baseball. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Balozi wa Japan
Nchini, Shinichi Goto wakati alipofungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha
Baseball na Kuzindua Mashindano ya Taifa ya Baseball, kwenye Shule ya
Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua
kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindu Mshindano ya Taifa ya
Baseball kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam,
Desemba 6, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimtambulisha Mkwe wa Jackie
Robinson, Muasisi wa Mchezo wa Baseball Duniani, Rutti David Robinson
(katikati) na Mjukuu wa Muasisi huyo, Busaro David Robinson (kulia)
wakati alipofungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua
Mashindano ya Taifa ya Baseball kwenye Shule ya Sekondari ya Azania
jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipofungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano ya Taifa ya Baseball kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018. Kulia kwake ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na kushoto kwake ni Balozi wa Japan Nchini, Shinichi Goto. Kushoto ni Mkwe wa Jackie Robinson ambaye ni Muasisi wa mchezo wa Baseball Duniani, Rutti David Robinson na wapili kushoto ni Mjukuu wa Muasisi huyo, Busaro Robinson. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipofungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano ya Taifa ya Baseball kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018. Kulia kwake ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na kushoto kwake ni Balozi wa Japan Nchini, Shinichi Goto. Kushoto ni Mkwe wa Jackie Robinson ambaye ni Muasisi wa mchezo wa Baseball Duniani, Rutti David Robinson na wapili kushoto ni Mjukuu wa Muasisi huyo, Busaro Robinson. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akirusha mpira huku Balozi wa Japan
Nchini, Shinichi Goto (kushoto) akijiandaa kuuzuia wakati Waziri Mkuu
alipofungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano
ya Taifa ya Baseball kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es
salaam, Desemba 6, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mmoja wa wadhamini wa
Ujenzi wa Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball, Dkt. Kazusue Konoike
wakati alipofungua kiwanja hicho na Kuzindua Mashindano ya Taifa ya
Baseball kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es slaam,
Desemba 6, 2018. Katikati ni Balozi wa Japan Nchini, Shinichi Goto.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
..................................................
..................................................
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua kiwanja kipya cha Taifa cha mchezo wa Baseball na kuzindua mashindano ya Taifa ya Baseball nchini.
Amewaagiza
viongozi wa Wizara ya Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni na Ofisi ya
Rais-TAMISEMI waone umuhimu wa kuuendeleza mchezo huo.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Desemba 6, 2018) alipofungua kiwanja
cha Baseball katika shule ya Sekondari ya Azania, jijini Dar es Salaam.
Amesema
iwapo mchezo huo utaratibiwa vizuri na kuingizwa katika
michezo UMISETA na UMITASHUMTA utaleta tija kwa wanafunzi wanaoucheza
nchini.
Waziri
Mkuu amesema thamani ya uwanja huo ni takribani Dola za Kimarekani
80.234 ambazo zimetolewa kwa msaada kutoka Serikali ya Japani.
Amesema
anaishukuru Serikali ya Japan na amefarijika kwa dhamira yao ya kuunga
mkono utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi CCM 2015-2020 hususan ibara ya
161.
Waziri
Mkuu amesema ilani inaielekeza Serikali kujenga na kuimarisha
miundombinu ya michezo nchini na kuifanya sekta ya michezo kutoa ajira
hususan kwa vijana.
“Pia
naishukuru Osaka Rotary Club ya nchini Japan kwa msaada wao wa dola za
Kimarekani 12,856 kwa kufadhili mashindano hayo ya sita ya mchezo wa
Baseball.”
Amesema
jitihada hizo zitaufanya mchezo wa baseball kuwa ni mmoja wa mchezo huo
kukua kwa kasi na unachezwa kuanzia ngazi za shule ya msingi na
sekondari.
“Nina
hakika baada ya hapo Tanzania itaweza kushiriki kwenye mashindano ya
kitaifa na kimaifaifa na hasa yale ya Olimpiki ya Tokyo Japan 2020.
Kadhalika,
Waziri Mkuu ameagiza uwanja huo ulindwe na utunzwe ipasavyo ili utumike
katika mashindano ya ndani na nje ili uwe sehemu ya kuitangaza nchi.
Awali,
Balozi wa Japan nchini, Balozi Shinichi Goto alisema nchini Japan
mchezo huo pia unasaidia katika kuwajenga vijana kukua kinidhamu na
kujiamini.
Alisema
anatarajia kwamba mashindano ya mchezo huo yatakuwa endelevu nchini na
wachezaji watacheza vizuri kutokana na uwepo wa uwanja mzuri.
Balozi huyo alisema mchezo huo unafundishwa na walimu wa Kijapani katika mikoa mbalimbali Tanzania Bara na Zanzibar.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, DESEMBA6, 2018.
Post a Comment