UJUMBE WA MBOWE KUTOKA GEREZANI HUU HAPA.
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe, amewataka wafuasi wake wasihuzunike na hatua ya yeye kuwekwa rumande kwa madai ya kutopatiwa dhamana bali watumie nafasi hiyo kuombea tume huru ya uchaguzi.
Kauli
hiyo ya Mbowe imetolewa Jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu wa
chama hicho bara na mbunge wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika wakati
akizungumza na waandishi wa habari kuelekea siku ya kusikilizwa rufaa ya
kupata au kutopata dhamana kwa viongozi hao wawili.
"Mwenyekiti
amesisitiza sana, kutomlilia yeye bali walilie taifa letu kutafuta
mabadiliko, kudai tume huru ya uchaguzi, kwa sababu kesi hii msingi wake
ni uchaguzi uliosababisha kifo cha Mwanafunzi wa NIT, Akwilina kwa hiyo
naomba wajitokeze kwa waingi kesho," amesema Mnyika.
Wakati
huohuo Mnyika amebainisha kuwa chama hicho kupitia mawakili wake
kimewasilisha maombi ya kuiomba mahakama kutoa kipaumbele kwa kesi dhdi
ya viongozi wake kabla ya mahakama hiyo haijaenda likizo.
Mbowe
na Matiko wako mahabusu baada ya kufutiwa dhamana kwenye kesi yao ya
msingi inayowakabili juu ya kusababisha kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa
NIT, Akwilina Akwilini ambapo walifutiwa dhamana hiyo kwa madai ya
kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Post a Comment