TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA VIWANDA AFRIKA,VIWANDA VYA KUONGEZA THAMANI MAZOA BADO KITENDAWILI.
Na John Luhende
Tanzania na imeungana na nchi nyingine za kiafrika katika
maadhimisho ya siku ya viwanda Afrika ,kwa kuwakutanisha wenyeviwanda na
wazalishaji wa bidhaa za viwandani
hapanchi.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkurugenzi msaidi idaraya maendeleo ya viwanda Wizara ya viwanda biashara na uwekezaji Mhandisi
Eli Paranjo , amesema Tanzania imedhamiria kwa dhati kujenga uchumi
wa viwanda na wameungana na nchinyingine
kusisitiza juu ya umuhimu wa viwanda kwa kuwa hauna maendeleo bila
viwanda na vinaongeza pato la nchi.
Amesema viwanda vinasaidia kuongeza thamani ya malighafi
ya mazao na madini na kuongeza mapato ya serikali , kuongeza ajira na
kuondoa umasikini , siku hii ilianzishwa na Umoja wa mataifa kwa kutumia
shirika la UNIDO ilikusaidia nchi za Afrika ambazo hazijaendelea ili
kuzihamasisha kujenga uchimi wa viwanda .
Serikali ya awamu
ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe
Magufuli imeweka nguvu kubwa katika
ktekeleza sera ya ya Maendeleo endelevu ya Viwanda
(1996 -2020) awamu ya tatu inayo
tekelezwa kwa kipindi cha 2010 -2020
ambayo inatekelezwa kwa mkakati unganishi
wa maendeleo ya Viwanda na mpango wa
pili wa maendeleo ya miaka mitano 2016/17 -2020/21 moja ya malengo ya
awamu hiyo ambapo ni kuiwezesha sekta ya
Viwanda kuleta mabadiliko ya uchumi
ili kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati.
Naye makamu
mwenyekiti wa wa shirikisho la wenye viwanda nchini CTI , Shubiza Bell ,ameshukuru UNIDO na TANTRADE kwa kuwakutanisha katika siku hii
na kuiomba serikali kufanyia kazi makubaliao waliofikia kuhusu taratibu za tozo
kwa taasisi zake ili viwanda vyao viweze
kuendelea na kujiendesha kwa faida tofauti na ilivyo hivisasa ambapo tozo
zimekuwa nyingi ukiondoa kodi ya serikali.
Post a Comment