MHE HASUNGA ASISITIZA MAWAZIRI JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUONGEZA MSHIKAMANO KWENYE SEKTA YA KILIMO Inbox x
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Katikati), Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina (Kushoto) na Waziri wa Kilimo, Mifugo, Maliasili na Utalii-Zanzibar Mhe Rashid Ally Juma wakiwa katika picha ya pamoja katika ukumbi wa mikutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha, Leo tarehe 7 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe Christophe Bazivamo, Waziri anayeshughulikia EAC nchini Burundi Mhe Isabelle Ndahayo, Waziri wa Kilimo nchini Kenya Mhe Mwangi Kiunjuri, Katibu Mkuu wa Kilimo nchini Rwanda Ndg Musabyimana Jean Claude, Waziri wa Kilimo Sudani Kusini Mhe Onyoti Adigo Nyikwec, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Tanzania Mhe Luhaga Mpina (Mb), Waziri wa Kilimo Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb), na Waziri wa Kilimo, Mifugo, Maliasili na Utalii-Zanzibar Mhe Rashid Ally Juma wakiwa katika picha ya pamoja katika ukumbi wa mikutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha, Leo tarehe 7 Disemba 2018.
Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo-Arusha
Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Mhe Japhet Hasunga amewataka mawaziri
wenzake wa sekta ya Kilimo kutoka nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki
kuongeza umoja na mshikamano ili kuakisi matakwa ya jumuiya katika Uzalishaji
wa bidhaa bora za Kilimo.
Waziri Hasunga ameyasema hayo Leo tarehe 7 Disemba 2018 wakati
akizungumza mara baada ya kumalizika mkutano wa 12 wa Baraza la kisekta la
mawaziri wa Kilimo na usalama wa chakula wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki
ikiwemo wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini.
Mhe Hasunga alisema kuwa kadri ushirikiano mwema utakavyoendelezwa ikiwa
ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii itaimarisha tija na mafanikio ya soko la
bidhaa katika jumuiya hiyo na dunia kwa ujumla.
Aidha, amewataka watendaji wote katika nchi za jumuiya ya Afrika
Mashariki kutekeleza taarifa mbalimbali zinazoandikwa kwa ustadi mkubwa kwani
kwa kiasi kikubwa kumekuwa na utekelezaji duni wa mipango hiyo.
Mkutano huo wa mawaziri wa sekta za Kilimo umetanguliwa na vikao vya ngazi
ya wataalamu na ngazi ya makatibu wakuu vilivyoanza tarehe 3 Disemba 2018.
Katika mkutano huo maeneo yaliyojadiliwa ni pamoja na kuhusu mchakato wa
CAADP katika Jumuiya hususani ripoti ya taaarifa ya utekelezaji wa Azimio la
Malabo na kupitisha Mkakati wa kuendeleza Sekta ya Kilimo na Chakula (REGIONAL
AGRICULTURE INVESTMENT PLAN - RAIP) sambamba na Programu ya kudhibiti sumukuvu
(aflatoxin prevention and control).
Maeneo mengine ni kuhusu Programu ya masuala ya afya ya
mimea na wanyama (SPS programme) hususani kuhusiana na biashara za kimataifa,
ushirikiano kati ya EAC na Marekani katika masula ya biashara ya mazao ya
kilimo, masuala ya pembejeo hususani mbegu na viuatilifu, Chakula na Lishe
Mawaziri wameridhia Mkakati na Mpango kazi wa kutekeleza masuala ya
Chakula na Lishe wa Jumuiya.
Mkakati na mpango huo utatekelezwa katika mipango na mikakati ya nchi
wanachama, Kwa Tanzania kupitia mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya
pili (ASDP II) na miradi mingine inayoendelea, Mradi wa kuhamasisha vijana
kujiajiri katika Kilimo ambapo Vijana watatu watatu kutoka nchi zote wanachama
watapokea tuzo za ushindi katika kujihusisha na kilimo.
Mjadala huo pia umehusu ripoti ya mifugo na samaki katika Jumuiya ambapo
Maeneo muhimu yaligusa udhibiti wa magonjwa ya wanyama yanayovuka mipaka,
Mkakati wa pamoja wa usimamizi wa magonjwa yanayoambukiza wanyama na binadamu,
Masuala ya uvuvi yamezingatia changamoto za uvuvi haramu na jinsi
zinavyoshughulikiwa, Sera ya uvuvi na ukuzaji wa viumbe kwenye maji.
Pia mkutano huo wa 12 wa Baraza la kisekta la mawaziri wa Kilimo na
usalama wa chakula wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki umejadili
kuhusu Utafutaji wa rasili za kutekeleza mipango na mikakati ya Jumuiya,
lakini Maeneo mengine ya muhimu yaliyojadiliwa ni pamoja na kirusi
kinachoathiri mahindi, viwavi jeshi, homa ya bonde la ufa kwa upande wa mifugo,
mabadiliko ya tabia nchi na namna ya kukabiliana nayo na masuala ya
umwagiliaji.
Vilevile Waziri Hasunga amesema kuwa mkutano huo umemalizika kwa
mafanikio makubwa ambapo mjadala kuhusu chakula na usalama wa chakula umekuwa
na tina kwani umegusa maslahi ya wananchi.
MWISHO.
Post a Comment