TRA YANG'ARA TUZO YA NBAA, WAPATA USHINDI WA JUMLA.
Mkurugenzi wa Fedha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dinah Edward (kushoto) akipewa tuzo kutoka kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji baada ya TRA kutangazwa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) kuwa washindi katika kutengeneza vitabu bora katika Mamlaka ya Serikali.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji (wapili kutoka kushoto) akimkabidhi tuzo ya jumla Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichele(kulia).
Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichele(wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TRA.
Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichele(wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TRA.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kushinda tuzo mbili ikiwemo mshindi wa jumla kutoka Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) ambazo zinatolewa kwa taasisi, kampuni pamoja na mashirika mbalimbali ambayo yamefanya vizuri katika kuandaa taarifa za fedha katika utendaji wao.
Tuzo hizo walizopata TRA ni kuandaa vitabu bora vya hesabu katika Mamlaka za Serikali pamoja na kuwa mshindi wa jumla katika kutengeneza vitabu bora vya hesabu kwa kufata viwango na utaratibu za kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada NBAA kuwatangaza TRA kuwa washindi wa jumla katika mashinda hayo, Kamshna wa TRA Charles Kichele, amesema kuwa ushindi huo umetokana na kutengeneza vitabu kwa kufata taratibu na viwango vya kimataifa vinavyotumika kutengeneza hasebu za serikali.
Kichele amesema kuwa vitabu vyao vimeonekana vizuri kuliko vitabu vinavyotoka mamlaka nyingine.
Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichele akizumgumza na waandishi wa habari baada ya TRA kutangazwa kuwa washindi wa jumla.
"Siri ya mafanikio yetu ni ushirikiano na kujituma katika utendaji wetu wa kazi, kuna wakati tunafanya kazi hadi muda wa ziada" amesema Kamishna Kichele.
Ameeleza kuwa jitiada za wahasibu wa TRA zimeweza kuwapa ushindi wa jumla katika kuhakikisha wamefanya kazi yao katika viwango vinavyo stahili.
"Nawashukuru wahasibu wangu pamoja na mkurugenzi wa fedha kwa kazi nzuri walizofanya hadi kutupatia ushindi huu" amesema Kamshna Kichele.
Katika hatua nyengine Kamshna Kichele amewataka wafanyabiashara kuwa na utamaduni wa kuandaa vitabu vyao kwa ubora, jambo ambalo litasaidia kuandaa taarifa za fedha kwa ufanisi na kuleta maendeleo ya kiuchumi katika utendaji wao.
"Ni vizuri mamlaka, taasisi, makampuni wakajitaidi kuandaa taarifa za fedha kwa kutimiza viwango ili waweze kufikia mafanikio ya TRA" amesema Kamishna Kichele.
Awali Mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo za NBAA, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji, amesema kuwa uandaaji wa taarifa za fedha kwa kufata utaratibu ni jambo la muhimu kutokana uchangia kuleta ufanisi katika uchumi.
Dk. Kijaji amesema kuwa kwa sasa ajenda kuu ya serikali ni maendeleo ya kufikia uchumi wa kati hadi kufika mwaka 2025.
"Kwa sasa tunapanga na kuangalia maendeleo ili kuhakikisha tunakuwa na uchumi mzuri" amesema Dk. Kijaji.
Ugawaji wa tuzo za NBAA zilizotambulika kwa jina 'Best presented financial statements for the years 20I7 zimefanyika Desemba 8 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Post a Comment