Ads

Naibu Meya Ilala aagiza kituo cha fahari kujenga shule


Na Heri Shaban
NAIBU MEYA wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto ameagiza kituo cha kulea Watoto cha fahari kujenga maadarasa  mapya ili wasajili darasa la kwanza katika shule yao.


Naibu Meya Kumbilamoto alitoa kauli hiyo Dar es salaam jana wakati wa mahafari ya kituo hicho cha kulea watoto kilichopo Jimbo la Ukonga wa wilayani Ilala.


"Mafanikio ya kituo chenu mazuri kwa watoto wenu ambao wamefanyiwa mahafali Leo katika kituo hichi nawaomba mumsaidie Rais John Magufuli katika Serikali sekta ya Elimu eneo la kutosha lipo jengeni madarasa ili watoto wasome wasitoke kwenda kusoma mbali "alisema Kumbilamoto.

Kumbilamoto alisema serikali ya awamu ya tano inaimiza watoto kusoma  hivyo atazungumza na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mwita Waitara ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ukonga akiwezeshe kituo hicho kipate kibali cha kujenga shule ya Msingi.

"Kituo cha Fahari nimefurahishwa na Mazingira ya kituo  chenu kama NAIBU MEYA ILALA nakuomba Mkurugenzi  wa Kituo hichi shirikiana na Wazazi ili watoto waweze kusoma "alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Fahari  Neema Mchau alisema  kituo cha Fahari kipo chini ya Taasisi  isiyo ya kiserikali ya Tuamke Maendeleo iliopo Gongolamboto Ulongoni Wilayani Ilala .

 Neema alisema kituo cha Fahari kilianzishwa mwaka 2014 kikiwa na watoto 32  kwa sasa kina watoto 111 wavulana 61 wasichana 50 na Walezi sita.


Akielezea mafanikio alisema kimesajiliwa 2018 chini ya Wizara ya USTAWI wa Jamii Jinsia Wazee na Watoto

Pia kituo kimekuwa kikitoa msaada kwa makundi ya Mazingira
 Magumu katika vituo mbalimbali  pamoja na shule za Serikali.


Akizungumzia changamoto  Ufinyu wa eneo    la kituo  kutokana na mahitaji ya huduma kuwa kubwa pia uelewa Mdogo wa Jamii kutojua umuhimu wa kituo pamoja na malezi kwa Jumla.

"Tunakupongeza mgeni rasmi kuja katika mahafali haya ya kituo kama kiongozi wa Serikali maelekezo uliotupa ya kufanya upanuzi wa kituo chetu tutashirikiana na Ofisi yako Naibu Meya, Ofisi ya Mkurugenzi na Mbunge Mwita Waitara ili kuweza kufanikisha watoto waweze kusoma elimu ya Msingi"alisema Neema.


No comments