Dkt. Kalemani: Mradi wa Bomba la Mafuta Uganda-Tanga haujasimama utekelezaji unaendelea
Hussein
Ndubikile
Mwamba wa
Habari
Serikali
imesema utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka (Hoima) Uganda hadi Mkoani Tanga
haujasimama na kwamba hatua za utekelezaji wa mradi huo zinaendelea na
Hayo
yamesemwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani baada
ya kumalizika Mkutano wa majadiliano ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa bomba
hilo uliomkutanisha na Waziri wa Nishati na Madini wa Uganda, Irene Muloni.
Amesema kuwa
utekelezaji wa mradi huo uko katika hatua nzuri na kwamba pande zote mbili
wamejadiliana na kukubaliana kuhakikisha unakamilika kwa wakati uliopangwa
pamoja na hatua za utkelezaji za mradi.
“ Mradi
haujasimama tunaendelea na utekelezaji tumekubaliana tukamilishe ndani ya
waakati tuliokubaliana pande zote mbili,” amesema Dkt. Kalemani.
Amebainisha
kuwa katika upande wa Tanzania tayari wamekamilisha tafiti ya tathmini ya
mazingira, ustawi wa jamii pamoja ulipaji fidia mkoani Tanga.
Dkt.
Kalemani amesema malengo ya majadiliano ya mkuano huo ni hatua za
utekelezaji wake ikiwemo usafirishaji wa mafuta ghafi kutoka Hoima
nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga na kuyauza nje za nje.
Ameongeza
kuwa mradi huo utakuwa manufaa kwa jamii na makampuni ya ndani na kusisitiza
bomba lina urefu kilometa 1435 huku kilometa 1115 zikiwa sehemu ya Tanzania.
Kwa upande Waziri
Muloni amesema watahakikisha watafikia makubaliano na makampuni ili yaweze
kusaini utekekezaji wa mradi ukamilike mwaka 2020 ilivyopangwa.
Amefafanua
kuwa ifikapo Januari 14 mwakani mkutano mwingine utafanyika nchini Uganda lengo
likiwa kujadiliana mambo yaliyobaki makampuni yaanze utekelezaji.
Post a Comment