Miaka mitatu ya Rais Magufuli Hospitali ya Rufaa Mkoa AMANA yatoa huduma za kisasa
Baadhi ya majengo ya HOSPITAL ya Rufaa ya Mkoa Amana iliyopo Wilayani Ilala Dar es Salam Picha na Heri Shaban
Na Heri Shaban
Mwambawahabari
WANANCHI waipongeza serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli katika kipindi cha miaka mitatu ya Uongozi wake kwa sasa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa AMANA wanapata huduma bora.
Wananchi hao walikuwa wakiongea katika mahojiano maalum na Mwandishi wa habari hizi wakati akielezea kwa upande wa sekta ya Afya jinsi Serikali na Wizara ya Afya ilivyosimamia katika huduma za Matibabu kwa Wananchi.
Akizunngumza hospitalini hapo Mmoja wa Wananchi Tatu Omary alisema kwa sasa Amana mpya kuanzia mapokezi na wahudumu wake wanatoa huduma nzuri.
"Mimi mkazi wa Segerea kwa sasa na familia yangu yote huduma zetu tunapata Amana hospitali huduma za Matibabu nzuri atwendi katika hosptali binafsi "alisema Tatu.
Alisema Serikali ya awamu tano katika miaka mitatu ya Magufuli huduma ya sekta ya afya kila siku katika hospitali za Serikali na vituo vya afya zinaendelea kuboreshwa.
Tatu aliwataka Wananchi wa Wilaya ya Ilala na maeneo ya Jirani watumie hospitali hiyo ya Serikali ambapo kwa sasa ni ya Rufaa.
Kwa upande wake Ashura Idd naye alipatiwa Matibabu katika hospitali hiyo alisema kwa sasa Amana huduma zao nzuri katika miaka mitatu ya JPM kweli tunajivunia mazingira safi ya hospitali pamoja na majengo ya kisasa pia Walinzi wanakagua wageni kwa ajili ya Usalama wa Wananchi na hospitali kwa Jumla.
Ashura alisema pia mapokezi ya hospitali hiyo nzuri imejengwa ya kisasa kama ulaya
Mgonjwa akifika kupokelewa na wahudumu kwa sare maalum
Pia Mwananchi huyo alipongeza Serikali katika hosptali hiyo kutenga chumba maalum namba tatu cha kupokea Kero na malalamiko.
"Nawapongeza viongozi
Wote na Watumishi wa Hospitali ya Rufaa Amana mpaka gari zinazoingia getini zinakaguliwa wakati wa kuingia na wakati wa kutoka na Askari maalum wa SUMA JKT "alisema Ashura.
Post a Comment