WAZEE WA KIMILA WA KIMASAI LAIGWANANI WAWEKA AZIMIO LA NAMALULU LA KUMSOMESHA MTOTO WA KIKE MPAKA PHD.
Na Mwandishi Wetu Simanjiro Manyara
Wazee wa kimila kutoka kabila la kimasai wamekubaliana
katika kikao chao na uongozi wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kumsomesha
mtoto wa kike mpaka kufikia ngazi ya elimu ya PHD katika azimio lijulikano kwa
jina la Namalulu lililotolewa mwaka huu ikiwa ni jitihada za kumuwezesha mtoto
wa kike na kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa vitendo vya
ukeketaji katika jamii hiyo.
Hayo yamebainika wakati wa ziara
ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndugulile alipokuwa akizindua kituo Maalum cha kuwasaidia wahanga wa vitendo vya ukeketaji cha
Shirika la NAFGEM kilichopo Orkesumeti Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Azimio la Namalulu limefikwa na Wazee hao wa kimila
mara baada ya kushamiri kwa vitendo vya ukeketaji katika jamii ya kimasai ya
Simanjiro mkoani Manyara na kuamua kukata shauri na kuanza kubadilika na kutoa
elimu ya kuachana na vitendo vya ukekeketaji katika jamii yao.
Akizunguzma na Wazee wa kimila kutoka kabila la kimasai
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile amewaambia wazee hao wa kimila kuendelea kushirikiana na Serikali na wadau
katika kupambana na vitendo vya ukeketaji ambavyo vinamkandamiza mtoto wa kike.
Dkt. Ndugulile amesisitiza kuwepo kwa Kamati za
Ulinzi kw\ Wanawake na Watoto katika
ngazi zote ili kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukeketaji vinavyofanywa
na jamii ya kimasai katika Wilaya ya Simanjiro.
Naibu Waziri amesema Serikali imeweka Mpango
Mkakati wa Kitaifa wa kutokomeza vitendio vya ukatili wa kijinsia dhidi ya Wanawake
na Watoto wa mwaka 2016/2017 mpaka 2021/2022 wenye lengo la kuweka mikakti ya
kuondokana na vitendo hivyo moaka nagzi ya kitongoji.
“Niseme tu Serikali tumejipanga na hatutokubali
vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji uendelee katika jamii zetu”
alisema Dkt. Ndugulile.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mtandao Kupambana na
Ukeketaji Simajiro Bw.Francis Selasini ameishukuru Serikali kupitia Naibu
Waziri Ndugulile kwa kushirikiana nao katika kuendeleza mapambano dhidi ya
vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa vitendo vya ukeketaji na mpaka sasa
wameweza kuwakoa mabinti 15 ambao wamewasaidia kuendelea na elimu na maabinti
wawili wapo vyuo vikuu.
Naye moja wa msichana aliyekimbia ukeketaji
na ndoa ya utotoni Nagalali Molell amesema kuwa Shirka la NAFGEM limemsaidia
kumsomesha na kufikia mpaka hapo alipo na kumuwezesha kumuajiri kufundisha
wasichana wengine kushona.
Post a Comment