DAWA YA WAKEKETAJI WATOTO WACHANGA YAJA.
Na Mwandishi Wetu Manyara
Dawa ya wale wanaofanya vitendo vya Ukeketaji kwa watoto wadogo na ukeketaji kwa ujumla nchini
inaelekea kupatikana kutokana na kukidhiri kwa vitendo vya ukeketaji vya aina
hiyo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipokuwa akizundua kituo Maalum cha kuwasaidia
wahanga wa vitendo vya ukeketaji cha Shirika la NAFGEM kilichopo Orkesumeti Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali inaendelea na mapambano dhidi ya vitendo
vya ukeketaji kwani inaonekana wahusika wamenzisha mbinu mpya za ukeketaji
baada ya watoto kupta elimu juu ya madhara ya ukeketaji na wengi wao kukimbia
kufanyiwa vitendo hivyo.
Naibu Waziri Ndugulile amezitaja mbinu mpya za ukeketaji ni pamoja na
kuwakeketa Watoto wachanga, kutofanya Sherehe wakati wa ukeketaji na kufanya
vitendo hivyo nyakati za usiku.
Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa Serikali haipingi mila na desturi zilizopo katika
makabila ndani ya Tanzania ila kusiwepo na mila zisizofaa ambazo zinaleta
ongezeko la vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa vitendo vya ukeketaji.
"Vitendo hivi havikubaliki katika Tanzania ya awamu hii tuongeze nguvu
katika kupambana na vitendo vya ukeketaji" alisisitiza Dkt. Ndugulile
Dkt. Ndugulile pia amewataka viongozi wa kimila kutoa ushirikiano kwa Serikali
na wadau katika kuunga mkono jitihada za Serikali katika kupambana na vitendo
vya ukeketaji katika maeneo yao.
"Ni aibu kubwa sana kwa kukeketa na kuwaozesha watoto wadogo ambao
tunawaharibia ndoto zao" alisisitiza Dkt. Ndugulile.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro ameahidi kushirikiana na wadau katika
kuendeleza mapambano dhidi ya vitendo vya ukeketaji Wilayani humo.
"Nikuahidi Naibu Waziri tutaendelea na mapambano dhidi ya vitendo hivi
hatutamuacha mtu salama " Alisisitiza Dkt. Ndugulile.
Kwa
upande wake Mkurugezi Mtendaji wa Kituo cha Mtandao wa Kupambana na Ukeketaji
Simanjiro Bw. Francis Selasini amesema Shirika lake liekuwa likiwasaidia watoto
wa kike wanakimbia vitendo vya ukektaji na kuwapa elimu ya ujasilimari na
kuwasomesha wale ambao hawakupayta nafasi ya kusoma na mpaka sasa wamefanikiwa
kusomesha mtoto mmoja wa kike ambaye amerudi na kuanza kuwafundisha wenzake.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiyo Mhandisi Zephania Chaula amesema Serikali yaWilaya
imeweka nguvu kubwa katika kupambana na vitendo vya ukeketaji katika Wilaya
hiyo na kuweka jitihada za kuondoka na mila zisizofaa zinazo mkandamiza mtoto
wa kike.
Naye
moja wa msichana aliyekimbia ukeketaji Nagalali Molell amesema avitendo vya
Ukeketaji bado vinaendelea ktika maeneo ya vijijini na elimu zaidi inahitajika
ili kuweza kuikomboa jamii hiyo kwani watoto wa kike wamekuwa wakikandamizwa kwa
kulazimishwa kuolewa kukuketwa na kutopata elimu sawa wa watoto wa kiume.
Post a Comment