Ads

WANANCHI WAAMASISHWA KUCHANGIA DAMU MARA KWA MARA.


Na Maria Kaira,Mwambawahabari

Ikiwa uwitaji wa damu bado mkubwa katika hospitali, Wananchi wameamasishwa kuwa na moyo wa kuchangia damu mara kwa Mara kwa lengo la kuwasaidia wagonjwa waliokuwa na uwitaji wa damu ili kuweza kuokoa maisha yao. 

suala la kuchangia damu liwe chachu Kwa jamii kwa ujumla kutokana na mahitaji ya damu bado yanaongezeka kila siku.

Hayo yamesemwa leo na Mchungaji wa taasisi ya  Manm ministries Evance   Sindano wakati alipotembelea hospitali ya Amana  kuwaona wagonjwa na kuwaombea, kutoa msaada,kufanya usafi pamoja na kuchangia damu. 


Pia amesema yeye na taasisi yake wataendelea na huduma hiyo ya kuwatembelea wagonjwa wenye uwitaji na kuweza kuwasaidia kadri Mungu atakavyowawezesha. 

Aidha  Dokta Majidi Mfaume amesema anaishukuru taasisi hiyo kwa kujitoa kwao kwa moyo,pia ametoa wito kwa taasisi nyingine kujitokeza kuchangia damu kwa kuwa uwitaji wa bado mkubwa.

"Bado jamii haijakuwa na mwamko wa kuchangia damu,kiwango cha damu tunachokipata ni Kidogo kuliko matumizi tunayoyatumia nawahamasisha wananchi kuchangia damu ili tuweze kuokoa maisha ya wananchi wanao itaji damu "amesema

Kwa upande wake mchangiaji damu Dr Faustine Mzungukanga amesema ukichangia damu unakuwa umejiwekea  hazina kwa Mungu kwa kuokoa maisha ya mwananchi mwenzio.

Megi George ametoa wito kwa jamii kuwa na moyo wa kusaidia wengine wasiojiwe, pia amesema wananchi wajitokeze kuchangia damu ili waweze kupata kadi itakayoweza kumsaidia atakapokuwa na uwitaji wa damu. 

Hata hivyo Kaimu Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Amana Anna Mussa ameishukuru taasisi hiyo kwa kujitoa kwao na kuziomba taasisi nyingine kuiga mfano huo.


No comments