MSTAHIKI MEYA ISAYA MWITA KUWA MGENI RASMI TAMASHA LA WAJASIRIAMALI.
Na Maria Kaira,Mwambawahabari
Katika harakati
za kumkomboa mwanamke kiuchumi na kuachana nadhana ya kuwa tegemezi katika
jamii inayowamzunguka.
Taasisi ya Motherhood
Tanzania kwa kushirikiana na Evelyn Munisi Foundation wameandaa tamasha
litakaloweza kuwakutanisha wanawake wajasiriamali mbalimbali na kuweza kuinuana kiuchumi .
Akizungumza leo
na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Taasisi ya Motherhood Tanzania Tina Ndonde
amesema tamasha hilo litafanyika Novemba 10 katika viwanja vya Hekima Garden
vilivyopo mikocheni na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es
salaam Isaya Mwita .
Pia amesema
lengo la tamasha hilo ni kumwinua mwanamke kiuchumi na kuweza kujitegemea
mwenyewe kwa kujishughulisha na kazi za ujasiriamali ili mwanamke ainuke
kiuchumi.
“ kauli mbiu
ya tamasha hilo " Mama shujaa ni mlinzi wa familia, tunajua ukimuinua mama
umeinua jamii kwa ujumla na ndio maana tunapambana katika kumkombea mwanamke
aweze kujitegemea”amesema
![](https://scontent.fdar5-1.fna.fbcdn.net/v/t1.0-9/11056562_911794188889239_3031084136354693823_n.jpg?_nc_cat=102&_nc_eui2=AeFi5IOq1XAi3SLqcCIL7wQWmVsfcy1nXT4gJYTKWswCdxB4UdCJRTHSijIcqUjfxZczUdTOoQPrx4ZRSPSWSAYXm8cnpj1rah37KzVAftORvg&_nc_ht=scontent.fdar5-1.fna&oh=ce4cdc70d075e02fd50271be640a3f91&oe=5C426C5C)
Kwa upande wake
mmiliki wa Evelyn Munisi Foundation, evelyn munisi amesema wamejikita hasa
katika kuwainua wanawake kwasababu kundi hilo ndio wahanga wakubwa sana kwenye
jamii.
“kupia jambo
hili tumeweza kufikia sehemu kubwa ya jamii hii ya wanawake wenye shida na tumeweza
kufanikiwa kuwainua na kujitegemea wenyewe”
Aidha Evelyn amesema Lengo la Tamasha hilo ni
kuwasaidia wajasiriamali wadogo wadogo ambao hawana usajiri wowote kwa
kuwasaidia kuwakutanisha na Sido,Tbs,Tfda ambao watahusika kuwashauri wajasiriamali
hao nini wafanye ili biashara zao ziwe na ubora huku wakiwaa na lengo la kuwainua
mwanamke kiuchumi
Hongera Sana Tina
ReplyDelete