Mbunge Bwege Amkomalia Waziri wa Ujenzi Bungeni
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isaac Kamwelwe, ameendelea kuwa katika wakati mgumu baada ya Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Suleiman Bungara (Bwege), kudai waziri huyo anamdharau Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Amesema
Waziri Kamwelwe alitembelea jimboni kwake na kumueleza miradi ambayo
Waziri Mkuu ameiridhia na Kamwelwe kutoa kauli iliyoonyesha ni kumdharau
Waziri Mkuu.
Bwege
alitoa kauli hiyo jana Alhamisi Novemba 8, bungeni jijini Dodoma wakati
akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka
2019/20, ambapo pia alisema alidhani ni yeye pekee aliyejibiwa vibaya
lakini alishangaa jana kumsikia Mbunge wa Mafia, Mbaraka Dau(CCM),
akitoa maelezo kama yake.
“Dau
alisema kitu kilichonisikitisha sana, Waziri Mkuu anachaguliwa na Rais
na anathibitishwa na Bunge, jana hapa Dau alimwambia waziri habari ya
boti, lakini akajibiwa majibu mabaya na Waziri wa Ujenzi, si mara moja
hii, kuna mradi wa maji (Jimbo la Kilwa) nikamwambia naye akanijibu
Waziri Mkuu nani, mimi namtambua Rais John Magufuli tu.
“Kuna
mtu mmoja anamdhalilisha (Waziri Mkuu) si desturi nzuri waheshimiwa,
huyu ni Waziri Mkuu asidharauliwe, sisi tukisema sana tunaitwa katika
maadili,” alisema Bwege.
Baada
ya kauli hiyo, Spika Job Ndugai, aliyekuwa akiongoza kikao hicho
alisema “Bungara uko katika shughuli yako ya uchonganishi wako ili watu
wagombane humu.”
Akijibu kauli hiyo, Bwege alisema; “Mheshimiwa Spika mimi nanukuu yaliyosemwa hapa jana( Jumatano).”
Katika
kikao cha Jumatano, Dau alidai Waziri Kamwelwe amekiuka agizo la Waziri
Mkuu la kupeleka Mafia meli iliyotolewa na mfanyabiashara Said Salim
Bakhresa, akidai ni maagizo ya kisiasa na kwamba suala la kupeleka meli
hiyo Mafia walilijadili na Waziri Mkuu na akakubali ipelekwe Mafia jambo
ambalo hata Profesa Makame Mbarawa aliyekuwa waziri wa wizara hiyo,
aliliridhia.
Post a Comment