DKT. MWAKYEMBE AIJIA JUU YANGA.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mh. Harrison Mwakyembe, amewataka Yanga kuacha utani juu ya uchaguzi na hivyo ni vema wakafanya kama walivyoagizwa.
Mwakyembe ameeleza hayo kutokana na baadhi ya wanachama kuja juu na kupinga wakisema hawataweza kufanya uchaguzi huo haswa kujaza nafasi ya Mwenyekiti.
Waziri amesema hataki kusikia sababu ambazo hazina na akieleza wao kama serikali hakuna sehemu yoyote waliyokosea kuitaka Yanga kufanya uchaguzi huo kwasababu haiwezi kuendeshwa bila uongozi.
Kutokana na baadhi yao kukataa, Mwakyembe amesema hataona sababu kuwafungia ili wakajifunze na mwisho wa siku iweze kuwa funzo kwa wengine ambao ni wabishi.
Hata hivyo tayari Yusuf Manji ambaye aliwahi kujiuzulu nafasi yake ameandika barua ya kurejea kwenye nafasi hiyo hivyo hakutakuwa na haja tena ya kujaza nafasi ya Uenyekiti.
Manji ameandika barua na kuituma kwa Baraza la Wadhamini na imesomwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo, George Mkuchika

Post a Comment