Benki ya Amana na TY Services Limited zaingia mkataba kuwawezesha madereva kumiliki vyombo vya moto
Hussein
Ndubikile
Mwamba wa
Habari
Benki ya
Amana na Kampuni ya TY Services Limited inayoendesha mtandao wa Taxify nchini zimesaini mkataba wa kuwawezesha madereva
wa mtandao huo kumiliki vyombo
vya moto.
Akizungumza
na wanahabari wakati wa utiaji saini mkataba huo leo jijini Dar es Salaam
Meneja Mkuu wa Kitengo cha Biashara cha benki hiyo, Dassu Mussa amesema Benki
ya Amana inaendeshwa kwa kuzingatia misingi ya kiislam hivyo uingiaji mkataba
huo ni sehemu ya mikakati ya kuifanya
kuwa benki kiongozi katika kutoa huduma
za kibunifu zenye lengo la kuinua jamii kiuchumi.
“ Uwezeshaji
utafanyika katika vikundi, hivyo madereva
watahaitajika kuunda kikundi cha madereva 10 ambao watadhaminiana
wenyewe,” amesema.
Amebainisha
kuwa dereva atatakiwa kuweka amana isiyopungua asilimia 10 ya thamani ya chombo
cha moto anachohitaji kuwezeshwa na
kwamba amana hiyo itatumika kama dhamana mpaka dereva atakapokamilisha
marejesho.
Amesisisitiza
kuwa dereva wa mtandao huo atatakiwa kuweka akiba ya Sh 15000 kila wiki ambayo
itakuwa kama dhamana hadi mwisho wa marejesho.
Amefafanua
kuwa dereva atafanya marejeshon kulingana na makubaliano na benki hiyo katika
kipindi kisichopungua miaka miwili huku akibainisha watazingatia vigezo
mbalimbali katika kutoa uwezeshaji ikiwemo dereva kuwa na uzoefu wa kutosha na
rekodi nzuri.
Kwa upande
wake Meneja wa Mtandao wa Taxify nchini, Remmy Eseko amesema mkataba walioingia
ni moja ya mikakati ya kuhakikisha wanatoa huduma ya usafiri kwa gharama nafuu na
kuwaongezea madereva kipato.
Amewahaimiza
madereva wanaotumia mtandao huo kuchangamkia fursa hiyo yenye lengo la
kuhakikisha wanamiliki vyombo vyao vya moto kupitia benki hiyo.
Aidha, amesema anaamini mtandao huo utatoa huduma bora kwa wale wote watakaotumia.
Post a Comment