CHADEMA Temeke wafanya sherehe kuondoka kwa Diwani wa Mtoni
Katibu wa umoja wa Madiwani wilaya ya Temeke Benjamini Ndalichako(Kulia) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati wa kutoa tamko la CHADEMA kuhusu diwani wa Kata ya Mtoni Benard Mwakyembe ,mbaye kajiunga chama cha Mapinduzi CCM (kushoto)Mwenyekiti wa Madiwani Claudias Togocho(.PICHA NA HERI SHAABAN)
Na Heri Shaaban
UMOJA wa Madiwani wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)wilayani Temeke wamefanya sherehe kufuatia kuondoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Kanda ya Dar es Salaam Benard Mwakyembe ambaye ni diwani wa Mtoni.
Tamko la CHADEMA lilitolewa Dar es Saalam leo na Mwenyekiti wa Umoja wa Madiwani Temeke Claudias Togocho wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Togocho alisema kuondoka kwa Diwani huyo kwenda kumuunga mkono Rais Magufuli sio cha kushangaza kwani ndani ya CHADEMA alikuwa sio msaada.
"Chama chetu, tumefurahishwa kuondoka kwake Benard Mwakyembe kwani alikuwa anatutenga aungi mkono juhudi za CHADEMA pia aliwai kuwatoa madiwani ndani ya chama "alisema Togocho.
Alisema chama hicho kitaimalika zaidi na kuongeza wanachama kufuatia kuondoka kwake .
Aidha alisema Chama hicho akina makundi ndio maana UKAWA wamechukua jimbo la Temeke.
Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa madiwani wilayani Temeke Benjamini Ndalichako,aliwataka wakazi wa Mtoni kuwa watulivu chama hicho kitawatafutia diwani mwingine .
Ndalichako alisema kwa sasa wanajimarisha vizuri ndani ya chama kwa kungeza wanachama na kuja kutetea kiti cha udiwani Kata ya Mtoni .
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake BAWACHA TEMEKE Sina Manzi alisema yeye ndio alimpokea awali akiomba kujiunga ndani ya chama hicho hivyo anafahamu vizuri.
Alisema kuwa ameona atoshi katika chaguzi zijazo ndio ameamua kukimbilia Chama cha Mapinduzi CCM akidai anakwenda kumsaidia Rais John Magufuli
Benard Mwakyembe alijiunga CCM Dar es Salaam jana,katika mkutano wa kufunga kampeni Jimbo la Ukonga wa kumnadi Mwita Waitara ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dkt.Bashiru Ally,wengine waliojiunga CCM jana diwani wa kata ya Mnyamani Shukuru Dege.
Post a Comment