Ads

WAGOMBEA SIMBA KUCHUNGUZWA.

Kamati ya Uchaguzi ya Simba, leo Jumapili inatarajiwa kuzipitia fomu za wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya klabu hiyo baada ya leo kuhitimisha zoezi la upokeaji fomu.

Simba inatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu Novemba 3, mwaka huu kwa kuchagua viongozi wa nafasi za mwenyekiti na wajumbe. Zoezi hilo lilionekana kusuasua kutokana na kigezo cha mgo­mbea kuwa na elimu ya kiwango cha digrii kuwashinda wengi hali iliyosababisha kuwa na wagombea wawili tu wa nafasi ya uenyekiti ambao ni Sued Nkwabi na Mtemi Ramadhani na wajumbe 19.

Mwenyekiti wa Kama­ti ya Uchaguzi Simba, Boniface Lihamwike alisema kuwa, hakuna muda wa kupoteza kwa sasa kwa kuwa utara­tibu upo wazi kama am­bavyo hawakuongeza siku za kuchukua fomu ndivyo itakavyokuwa wakati wa kurudisha fomu.

“Tulitoa siku tano kwa ajili ya kukamilisha zoezi la ujazaji wa fomu ambapo mwisho wake ni Jumamosi ambayo ni tarehe 15 (jana) hivyo wale wote waliochukua fomu wanapaswa warejeshe ili tuweze kuendelea na mchakato wa uchaguzi kwa mujibu wa sheria.

“Siku tatu zitakuwa maalumu kwa ajili ya kuzipitia fomu na muda mwafaka kwa ajili ya kuweza kutazama wale wenye pingamizi na wa­takaokata rufaa baada ya kumaliza hatua hiyo kitakachofuata ni kutangaza wale am­bao wamekidhi vigezo na masharti,” alisema Lihamwike

No comments