WAITARA ATOA NENO BAADA YA KUTANGAZWA MSHINDI WA KITI CHA UBUNGE UKONGA

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam, Mwita Mwikabe Waitara (CCM) ameibuka mshindi wa kiti hicho baada ya kupata kura 77,795 sawa na asilimia 89.1 huku mpinzani wake, Asia Daudi Msangi ( CHADEMA) akipata kura kura 8,676 sawa na asilimia 9.95.
Baada ya kutangazwa kama mshindi wa uchaguzi mdogo wa marudio katika jimbo la Ukonga kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Mwita Waitara, amesema mawakala wa CHADEMA katika vituo vya kupigia kura walimpigia yeye.
Akiongea
leo baada ya kutangazwa, Mwita amesema alikuwa na matarajio ya kushinda
kwa zaidi ya asilimia 95, hivyo hajashangaa kupata ushindi huo wa
asilimia 89.
''Nina
ushahidi wa ujumbe mfupi kwenye simu yangu, mawakala wa CHADEMA katika
vituo jana wamenipigia kura na walikuwa wananitumia matokeo mapema tu
hiyo inaonesha nilikuwa na uungwaji mkono mkubwa sana'', amesema.
Aidha
Mwita amekishauri chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
kujitazama kilipojikwaa na sio kilipo angukia huku akiweka wazi kuwa
kama wanataka chama kibakie waachane na mwenyekiti wao Freeman Mbowe na
wakiendelea kumkumbatia chama kitawafia.
Akitangaza
matokeo ya uchaguzi leo, msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo hilo, Jumanne
Mashauri amemtaja Mwita Waitara wa CCM kama mshindi wa kiti cha ubunge
baada ya kupata kura 77,795 sawa na asilimia 89.1 huku mpinzani wake,
Asia Daudi Msangi ( CHADEMA) akipata kura 8,676 sawa na asilimia 9.95.
Post a Comment