Ads

Wanafunzi wa Shule za msingi 217,562, wanatarajia kupewa kinga dhidi ya Minyoo na Kichocho Wilayani Ilala.



Mwambawahabari
Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Ilala Jabir Makame akizunngumza katika ufunguzi wa kikao cha uhamasishaji kuhusiana na utoaji wa dawa ya kinga Tiba kichocho na minyoo ya tumbo MANISPAA ILALA Dar es salaam Leo ,ambapo jumla ya wanafunzi 217,562 wa wilaya ya Ilala wanatarajia kupatiwa chanjo hiyo kesho,zoezi litakalofanyika shule zote za Manispaa ya Ilala (kushoto) Mganga mkuu wa Manispaa ya Ilala Dkt. Emily Lihawa (PICHA NA HERI SHAABAN)


Mganga mkuu wa Manispaa ya Ilala Dkt Emily Lihawa (Picha na Heri Shaban)

Na Heri Shaban
MANISPAA ya Ilala Dar es salaam Leo imeanza kampeni ya utoaji chanjo ya magonjwa yaliokuwa hayapewi kipaumbele kwa shule zake za MSINGI zote za Serikali pamoja na binafsi.

Lengo la kutoa chanjo hiyo kuzuia watoto hasa wanafunzi wasipatwe na magonjwa hayo kutokana na Kitumia maji ya katika madimbwi na mabwawa.

Akingumza Dar es salaam Leo Mganga Mkuu wa Manispaa Ilala Dkt Emily Lihawa katika uzinduzi wa Kampeni hiyo Wilaya ya Ilala katika kikao cha Uhamasishaji (PHC)  Kuhusu utoaji wa dawa kinga tiba, kichocho na minyoo ya tumbo alisema Manispaa hiyo imeanza zoezi hilo kufuatia kutoa elimu kwa Mwalimu Wakuu wa Shule zote.

"Mpango huu wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliokuwa hayapewi kipaumbele katika wilaya yangu tumeanza kampeni ya utoaji chanjo Leo Mara baada kutoa elimu kwa walimu na lengo kuu kuwafikia wanafunzi wote matarajio kuwafikia wanafunzi 217,562"alisema Dkt. Emily.

Dkt Emily alisema hayo yanaathiri zaidi Jamii zinazoishi katika hali ya umasikini pasipo na hali ya usafi wa mazingira na wamezunguukwa na wadudu wanaosambaza magonjwa hayo.

Alisema Jamii hizi Mara nyingi hazina hata uwezo wa kugharamia Matibabu yao wanapougua, hivyo uleta umasikini katika JAMII  ,makuzi ya watoto huathirika huleta maumivu ya muda mrefu na hata ulemavu na uleta unyanyapa.


Alielezea ukubwa wa tatizo kidunia alisema watu zaidi ya bilioni 2,7 wanaishi katika mazingira ya umasikini wenye kipato cha chini ya dora za kimarekani wameathirika na magonjwa hayo.


Aidha alisema magonjwa hayo yasiopewa kipaumbele upatikana zaidi maeneo ya vijijini katika miundombinu duni na sehemu za mijini zenye msongamano mkubwa wa watu na nchi ambazo zinamachafuko ya kisiasa.


Kwa upande wake Mratibu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele MARTIN Karongolera alisema madhara ya magonjwa hayo kwa Jamii upatwa na ulemavu wa muda mrefu, kuathitika makuzi ya Mtoto, kuharibika kwa mimba, hupunguza uwezo wa kufanya kazi, hivyo uleta umasikini kwa mtu binafsi, Jamii, na nchi nzima.

Pia unyanya paa hasa kwa wasichana wa kike, ,utapiamlo kwa watoto, upungufu wa damu mwilini na udhaifu unaoweza kusababisha Maradhi.

Naye mgeni rasmi Kaimu KATIBU TAWALA wa wilaya ya Ilala Jabir Makame aliwataka wadau kushiriki kikamilifu katika kutoa elimu ya kuhamasisha Jamii ili Kila Mtoto apate fursa hiyo kwa ajili ya AFYA yake.

No comments