Madiwani Watano wa CHADEMA, CUF Watimkia CCM
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
Madiwani
watano wa vyama vya upinzani ikiwemo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA, CUF na ACT Mzalendo na viongozi wengine sita wamevikimbia
vyama hivyo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Pwani.
Madiwani
hao ni pamoja na Ramadhan Lutambi aliyekuwa diwani wa kata ya Mailmoja
kupitia Chadema na Ramadhan Kombe aliyekuwa diwani kata Mbwawa kupitia
ACT.
Wengine
ni, Muharami Mkopi Cuf kata ya Ruaruke wilayani Kibiti,Seif Lwambo
kupitia Cuf kata ya Beta,Muharami Mketo Cuf Kata ya Lukanga na
Mwenyekiti wa Kijiji cha Lukanga.
Aidha
viongozi waliojiuzulu kwenye vyama hivyo ni Ayubu Chapile ambae alikuwa
katibu kata ya Mkuza (CUF) ,Karimu Kasimu katibu tawi chuo kikuu cha
Mwalimu Nyerere (Chadema) ,Selemani Mwinyimkuu mwenyekiti tawi
(Cuf),David Mramba Act,Latifa Sangalala mwanachama Chadema Mkoani B na
Jumanne Urembo Diwani kivuli ACT kata ya Sofu.
Awali
Ramadhani Lutambi alisema ,chama kinachofaa kuongoza nchi daima ni CCM
kwani vyama vingine havina uwezo,na havijali viongozi wa ngazi za chini
.
Alifafanua ,ameamua kuondoka Chadema ili kutekeleza yale yanayofanywa na Rais Dk. Magufuli kwa wananchi wanyonge.
Lutambi alikiri kuondoka Chadema kwa hiari yake, kwa akili zake timamu na kudai anajivua vyeo vyote alivyonavyo kuanzia sasa.
Akiwapokea
madiwani na viongozi wa vyama hivyo kwenye ofisi za CCM Mkoa,
mwenyekiti wa CCM mkoani Pwani, Ramadhani Maneno alisema ,kutokana na
utekelezaji mzuri wa ilani wameona hakuna sababu ya kubaki kwenye vyama
vyao.
Alisema
kazi kubwa inayofanywa na chama kupitia Rais Dk .John Magufuli ndio
sababu kubwa ya madiwani na viongozi hao kukimbilia CCM.
“Baadhi
ya watu wamekuwa wakipotosha kuwa wabunge,madiwani na viongozi
wanaohamia CCM wananunuliwa ,suala hili halipo ,ni kwamba wanarudi
kutokana na utendaji kazi wa chama chetu,” alisema Maneno.
Maneno alieleza, viongozi hao hawanunuliwi wala kuhongwa bali ni mapenzi yao .
“Kuhusu
gharama za uchaguzi kuwa ni kubwa hilo ni suala la Tume ya uchaguzi na
chama kisilaumiwe kwani kuhama kwao hakuhusiani na kurubuniwa ,” alisema
Maneno.
Post a Comment