Ads

LHRC YAZINDUA RIPOTI YA NUSU MWAKA, MATUKIO YA UKATILI WA KINGONO YAONGEZEKA.

Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Serikali imetakiwa kuendelea kudhibiti matendo ya ukatili ambayo yamekuwa yakifanyika katika jamii na kusababisha ukosefu wa haki za binadamu.

Matukio hayo ya ukatili dhidi ya Watoto na wanawake  yamezidi kuongezeka katika kipindi cha miezi 6 kuanzia januari mwaka huu ukilinganisha na mwaka 20I7.

Akitoa taarifa ya Ripoti ya nusu mwaka ya Haki za Binadamu leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa  Kituo cha Sheria na Haki za binadamu (LHRC) Anna Henga, amesema kuwa  kuna ongezeko kubwa la ukatili dhidi ya Watoto.

Henga amesema kuwa ripoti hiyo imebaini kuwa kumekuwa na ukatili wa kingono ambao umezidi kuongezeka, kwani watoto I2 mwaka 20I7 walifanyiwa ukatili na idadi hiyo kuongezeka na kufikia 533 kwa mwaka huu.

Amesema kuwa kati ya matukio 6376 ya ukiukwaji wa haki za watoto, matukio 2365 yametokana na ubakaji huku 533 yakiwa ya ulawiti.

Henga amefafanua kuna mambo mengine ambayo yameonekana katika ripoti hiyo ikiwemo kuongezeka kwa ukatili dhidi ya wanawake, kwani imeripotiwa katika kipindi cha mwezi January hadi june mwaka huu wamekuwa wakiripotiwa kubakwa.

Hata hivyo ameeleza kuwa kwa sasa kumepungua kwa mauwaji yanayotokana na imani za kishirikina pamoja na kujichukulia sheria mkononi.

"Pia ripoti imeonesha ajali za barabarani pamoja vifo vinavyotokana na ajali hizo vimepungua" amesema Henga.

Katika hatua nyingine Henga amezitaka Mamlaka mbalimbali za serikali ikiwemo Jeshi la polisi kutumia njia mbadala ili kuhakikisha vitendo vya ukatili vinazibitiwa ipasavyo.

Ripoti ya nusu mwaka ya LHRC imeandaliwa kwa kutumia vyanzo mbalimbali ikiwemo taarifa za Jeshi la Polisi, ripoti za mashirika mbalimbali, vyombo vya habari pamoja na taarifa zinazopokelewa na vitengo vya LHRC.

No comments