KENYA KUUZA MAPARACHICHI AFRIKA KUSINI
Kenya sasa inaweza kuuza maparachichi nchini Afrika Kusini. Nchi hiyo imefungua soko la matunda hayo lililolifungwa kwa takribani miaka 11 iliyopita.
Hatua hiyo, imetokana na mazungumzo yaliyofanywa na wawakilishi wa serikali za nchi hizo mbili wakiwemo mawaziri wanaohusika na kilimo na biashara.
Mamlaka ya udhibiti wa bidhaa nchini Afrika Kusini iliweka zuio la kufanyabiashara ya maparachichi na Kenya baada ya kugundulika kuwepo kwa mdudu anayejulikana kama Bactrocera Invadens).
Mdudu huyo anayeaminika kutokea katika nchi za Asia, alionekana kwa mara ya kwanza nchini Kenya mwaka 2003 na kusambaa na kuathiri mazao mengi ya matunda nchini humo.
Soko hilo jipya la maparachichi baina ya nchi hizo mbili, lilifunguliwa rasmi Julai 24, mwaka huu na mamlaka nchini Afrika Kusini kwa kuandika barua kwa Waziri wa Kilimo na Biashara nchini Kenya.
Mapema, katika jitihada za kufungua soko hilo Kenya ilitakiwa na Afrika Kusini kuitengeneza maeneo ya mashamba yasiyoathiriwa na wadudu na kuyatengeneza mazingira ya ubaridi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Sera kutoka Wizara ya Kilimo, John Mwaniki Kenya ilibidi ikitane na mamlaka nchini Afrika Kusini kuzungumzia suala hilo la kufungua soko la maparachichi ambapo mazungumzo hayo yalifikia muafaka.
Post a Comment