Ads

UWT Wilaya Temeke wampongeza Rais Magufuli

 Mwambawahabari
  Heri Shaban
UMOJA wa Wanawake Wilaya ya Temeke  wamefanya sherehe ya kumpongeza Rais John Magufuli kwa ununuzi wa ndege mpya ya nne ambayo itakuwa inasafiri masafa marefu .

Pongezi hizo zilitolewa Dar es Salaam jana na Katibu wa Umoja wa wanawake UWT WILAYA ya Temeke Kimenta Mavala wakati wa hafla fupi iliyofanyika ofisi za CCM Wilaya Temeke ambazo zimeandaliwa na UWT.

"Sisi kama wanawake wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT wilaya ya Temeke tunakupa pongezi kubwa  kwa kuhakikisha unatekekeza ahadi ya ununuzi wa ndege ya nne kati ya Saba "alisema Mavala.

Mavala alisema UWT wilaya Temeke inamuomba Rais aendelee kutimiza ahadi kama zilivyoainishwa katika ilani ya Chama cha mapinduzi CCM.

Aidha UWT Temeke imemshauri Rais John Magufuli aendele kurudisha nidhamu ofisini ususani upande wa Wanawake.

Pia wamempongeza kwa mapambano dhidi ya ufisadi, rushwa katika Jamii na kumuomba aendelee na mapambano hayo kuakikisha wanawake wanajikomboa katika umasikini, hususani wanawake ambao wanaendelea kukosa huduma za msingi za kijamii ikiwemo afya  ,maji, na malazi bora.

Ametoa rai kwa watanzania kumuunga mkono Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania sambamba pia kujivunia uraia wa Tanzania.

Alisema wanamuombea kwa Mwenyezi Mungu azidi kumpa afya njema,Moyo wa ujasiri upendo na uzalendo kwa Watanzania.


Akizungumzia uhai Katika jumuiya hiyo alisema UWT Wilaya ya Temeke jumla wanachama 42,612 kati ya wanachama hao hai 39,212 .

Kuhusu jumuiya kwa sasa ipo vizuri  wanachama wanalipa ada kwa wakati na wanachama wanaendelea kujiunga kila siku.

Alimpongeza Makamu wa Rais kwa uanzishwaji wa majukwaa ya Wanawake na kuomba
Viongozi wa MANISPAA ya Temeke kutoa elimu hiyo ili iwafikie Wanawake wote wajue nini maana ya jukwaa na faida zake na fursa zilizopo .

Changamoto nyingine fedha za TASAF azifikii walengwa waliokusudiwa na Katika vituo vya afya dawa zilizopo chache.

No comments