Majibu ya Polepole kwa CHADEMA

Chama
cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakina wasiwasi wa aina yoyote na Tume ya
Uchaguzi (NEC) katika uchaguzi mdogo wa marudio wa Ubunge katika Jimbo
la Buyungu mkoani Kigoma huku kikidai waoitilia shaka tume hiyo wao ndio
wenye matatizo.
Hayo
yamelezwa na Katibu Mwenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole baada ya
kupita takribani siku tatu tokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kutoa kauli yake iliyokuwa ikiitaka NEC kuendesha uchaguzi huo
kwa uhuru na haki kuwa kuna baadhi ya vitu wamevibaini vikiendeshwa
ndivyo sivyo.
"Sisi
hatuna mashaka yoyote na Tume ya Uchaguzi (NEC) na kama tungekuwa nayo
basi tungeshayaeleza mahali husika ila ukiona mtu anajitokeza barabarani
na kusema kuna changamoto bila ya kuzipeleka sehemu husika basi ujue
yeye ndiyo mwenye changamoto nasio Tume", amesema Polepole.
Pamoja
na hayo, Polepole ameendelea kwa kusema "Chama cha Mapinduzi
kimejiwekea rekodi ya kushughulika na shida za watu na kutatua kero za
wananchi wa Tanzania na hili limefanyika vizuri sana chini ya serikali
ya CCM inayoongozwa na ndugu John Magufuli. Tumekuwa hatuna mzaha,
masihara na watu wanaocheza na rasilimali za umma, wanaonyanyasa
wananchi, wasiowajibika na kushughulika na shida za watu na kwa rekodi
ambayo tumeshajiwekea mpaka sasa hivi tutaenda kupanda ushindi mkubwa wa
kishindo kwasababu ya kazi ile nzuri ambayo tumekwisha ifanya hadi sasa
hivi".
Uchaguzi
huo mdogo wa marudio umepangwa kufanyika Agosti 12 mwaka huuu baada ya
kuwepo wazi Jimbo la Buyungu Mkoani Kigoma kufuatia Mbunge Kasuku Bilago
kufariki dunia mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu pamoja na madiwani wa
maeneo mbalimbali kuyaacha majimbo yao na kujiunga CCM kwa lengo la
kumuunga mkono Rais Magufuli.
Post a Comment