Huyu hapa Mwamuzi wa fainali Ufaransa Vs Croatia

Shirikisho
la Soka Duniani (Fifa), limemtaja mwamuzi atakayechezesha mchezo wa
fainali wa Kombe la Dunia, Ufaransa dhidi ya Croatia, utakaoshuhudiwa
kwenye uwanja wa Luzhniki nchini Urusi, Jumapili hii.
Nestor
Pitana ambaye ni raia wa Argentina mwenye uzoefu, ndiye atakayepuliza
kipyenga ndani ya dimba Jumapili hii ikiwa ni mechi yake ya tano nzito
kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Pitana
mwenye umri wa miaka 43 amepata nafasi hiyo kutokana na historia yake
ya kumudu mechi ngumu, akianza na mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji
Urusi na Saudi Arabia kwenye uwanja huohuo.
Anakuwa
mwamuzi wa pili kutoka Argentina kuchezesha mechi kubwa zaidi kwenye
ulimwengu wa Soka akimfuatia Horacio Elizondo aliyeweka rekodi mwaka
2006.
Pitana
alikuwa kwenye jopo la waamuzi kwenye Fainali za Kombe la Dunia nchini
Brazil miaka minne iliyopita, na hii itakuwa mechi ya tano, akiwa na
rekodi nzuri alipochezesha mchezo wa robo fainali kati ya Ufaransa na
Uruguay.
Wadau wa soka wamemteta Pitana, wengi wakionekana kumkubali kutokana na historia yake nzuri.
Mugabe amuahidi mpinzani mabilioni, magari kuendeshea kampeni
Mchezaji
wa Croatia, Ivan Rakitic amemzungumzia Pitana akikumbuka alivyoumudu
mtanange kati ya kikosi cha timu yake dhidi ya Denmark kwenye hatua ya
mzunguko wa timu 16.
“Nilifurahi
kusikia atakuwa mwamuzi wa fainali. Tulikuwa na bahati kumuona
akichezesha mchezo kati yetu na Denmark. Sio tu kwamba tulishinda lakini
alikuwa vizuri. Wasaidizi wake pia walikuwa wazuri sana,” amesema Ivan
Rakitic.
Pitana
atasaidiwa na waamuzi wa pembeni Hernan Maidana na Juan Pablo Belatti.
Massimiliano Irrati wa Italia atasimamia upande wa uamuzi wa kutumia
video, Video Assistant Referee (VAR).
Post a Comment