Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala wakabidhi photocopy mashine shule ya Mchikichini
Na Heri Shaban
Mwambawahabari
JUMUIYA ya Wazazi WILAYA ya Ilala wakabidhi mashine ya kurudufu photopy na kompyuta katika shule ya msingi Mchikichini.
Msaada huo ulitolewa na mlezi wa Shule hiyo Katibu wa Malezi na mazingira Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Ilala Wilison Tobola katika ziara yake endelevu ya kutatua changamoto mbalimbali katika sekta ya elimu na jumuiya hiyo.
"Mimi kama Katibu wa Malezi wilaya awali nilitoa ahadi katika shule hii baada kukuta changamoto leo nimetekeleza vile nilivyoaidi ili waweze kupriti mitihani kukuza taaluma katika Shule hii "alisema Tobola.
Tobola alisema ataendelea kushirikiana na Wazazi na Walimu wa Shule hiyo kama sehemu ya kuisaidia Serikali katika kuweka mazingira bora ya sekta ya Elimu Msingi ya elimu bure katika kimsaidia Rais John Magufuli.
"Jumuiya yetu ya Wazazi ipo imara imebeba jukumu la kuwa walezi Mimi Katibu wa malezi na mwenzangu Mjumbe wa CCM Mkutano Mkuu mkoa Dar es Salam,Azim khan tutashirikiana kila jambo katika Shule hii "alisema
Tobola alisema atashirikiana na Wazazi wa watoto wanaosoma shule hiyo kuweka Mpango mkakati watoto wawe wanafanya mitihani ya majaribio ili kuwajengea mazingira mazuri ya ufaulu.
Kwa upande wake Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam (CCM) Azim Khan alisema atashirikiana na Katibu wa Malezi wilaya ya Ilala ili kutatua changamoto zote za Shule hiyo.
Azim alisema jumuiya ya Wazazi wilaya YA ilala imeweza kuweka alama katika Shule hiyo kwa kutatua kero na kuweka Mazingira mazuri ya Shule.
Naye Mwalimu mkuu wa shule hiyo Wilson Mahemba alishukuru kwa kupokea Masada huo ambapo awali ilikuwa kero kubwa na kulazimika Kitumia fedha nyingi katika kuandaa mitihani ya majaribio lakini kwa sasa itakuwa unaandaliwa shuleni hapo.
Mahemba alisema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 504 Kati yao wavulana ni 257 na wasichana ni 247 Shule hiyo ni miongoni mwa Shule kongwe hapa nchini iliyoanzishwa mwaka 1939.
Alisema shule hiyo inachangamoto mbalimbali uchakavu wa miundombinu na ukuta wa kuzunguuka eneo la shule Jambo ambalo linapelekea kuwepo kwa kero nyingi na mazingira hatarishi kwa wanafunzi.
Mwisho
Post a Comment