CUF Ya Lipumba Yasema Itashiriki Uchaguzi Mdogo Uliotangazwa
Naibu
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya ambaye ytuko
upande wa Profesa Lipumba amesema chama hicho kitashiriki uchaguzi wa
ubunge katika majimbo ya Buyungu, Jangombe na kwenye Kata 79.
Akizungumza
jana Sakaya alisema chama hicho kimepokea barua kutoka Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC), kikielezwa kuwa majimbo na kata hizo, yapo wazi.
Alisema kutokana na mabadiliko yaliyofanyika NEC na katika vyombo vya Dola ni wazi kuwa wataibuka na ushindi katika chaguzi hizo
“Naomba
ifahamike kuwa CUF ipo moja na uamuzi wa chama ni kushiriki uchaguzi,
wanachama wasisikilize maneno ya watu ambao hawahusiki na chama,"
alisema Sakaya.
Alisema
wapo wanaojitambulisha kuwa viongozi wa CUF wanasema hawatoshiriki, si
kweli wamachama na wenye nia ya kutaka kugombea ubunge na udiwani
wajitokeze.
"Uchaguzi
wa ubunge jimbo la Kinondoni tulilalamikia utaratibu ulivyokuwa na
namna NEC walivyokiuka. Ila kw amabadiliko yaliyofanyika sasa, naamini
hali itakuwa nzuri,” alisema Sakaya.
Post a Comment