Mbunge Anatropia ataka Serikali itoe mikopo kwa wavuvi
Mbunge WA Viti maalum (CHADEMA) Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ANATROPIA Theonest (kushoto) akizungumza na mamalishe wa soko la samaki feri Dar es Salaam Jana katika ziara ya kikazi kuangalia changamoto za soko hilo (PICHA NA HERI SHAABAN)
MBUNGE wa viti Maalumu (CHADEMA) Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Anatropia Theonest akipika mboga Dar es Salaam jana, katika ziara yake ya kikazi kutembelea soko la samaki feri (PICHA NA HERI SHAABAN)
mbunge wa viti maalum Halmashari ya Manispaa ya Ilala Anatropia Theonest (Katikati) akiwa katika ziara kutembelea soko la samaki feri Dar es Salam jana kuangalia changamoto wanazokutana nazo wafanyabiashara katika soko hilo la kimataifa ,wengine ni Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Mwamba wa habari
Na Heri Shaban
MBUNGE wa Viti Maalum(CHADEMA)Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ANATROPIA Theonest ameiomba Serikali kuwapa mikopo wavuvi wa Samaki ili waweze kununulia vifaa vyao vya uvuvi waweze kuvulia samaki .
Ushauri huo umetolewa Dar es Salaam jana na Mbunge Anatropia katika ziara yake endelevu ambayo imeanza jana wilayani Ilala.
"Tunaomba Serikali iwekeze mikopo kwa kuwapa wavuvi ili wakanunulie vifaa vya uvuvi wa samaki wananchi wapate bidhaa hiyo kwa wakati "alisema Anatropia.
Anatropia alisema yeye ni Mbunge wa viti Maalum Halmashauri ya Manispaa ya Ilala hivyo ziara hiyo ina lengo la kuangalia changamoto ambazo wanakutana wananchi wake ndani ya Manispaa hiyo.
"Ziara yangu katika soko la Kimataifa la samaki Feri imebaini uchache wa samaki wateja hawapati samaki kwa wakati kutokana na vifaa duni vya uvuvi hivyo nashauri halmashauri ikielekezwa mikopo kwa wavuvi itawasaidia kukuza mitaji yao fedha hizo za mkopo wanunulie vifaa vya kuvulia samaki na kuboresha biashara zao.
Alisema changamoto nyingine alitopokea wafanyabiashara wanalalamikia tozo ya ushuru wa sh, 1000 kwa siku kubwa wameomba washushiwe tozo hiyo kutokana na gharama za maisha kupanda na hali ya biashara sio nzuri kwa sasa.
Aidha pia ameshauri Serikali kufanya upanuzi wa soko hilo ili lingizie mapato kwa Serikali kutokana na nafasi ndogo hasa upande wa MAMA Lishe na BABA Lishe eneo finyu lililopo kwa sasa .
"Eneo la MAMA Lishe inatakiwa wafikiliwe watengewe eneo la Majiko ya kupikia Mazingira ya kazi yao si salama yaliopo katika soko hilo"alisema
Kwa upande wake Meneja wa soko la Samaki feri,Mkuu Hanje alisema suala la wafanyabiasha kulipa ushuru wa sh, 1000 kwa siku lipo kisheria wasilalamike .
Meneja Hanje alisema kwa sasa viwango vya ushuru vimepungua wameunda Bodi ya soko la samaki feri toka mwaka 2017 ndio imepewa jukumu la kuratibu changamoto Zote sokoni hapo,kwa sasa soko linajiendesha kila jambo linashughulikiwa na Bodi hiyo ilioundwa.
"Bodi yetu iliyoundwa 2017 ndio inaratibu shughuli zote za soko la kimataifa feri, Changamoto kubwa vifaaa duni vya wavuvi vya kuvulia samaki inawafanya wateja kuchelewa kupata samaki kwa wakati "alisema Hanje.
Kwa upande wa usafi kwa sasa soko hilo limeboreshwa vizuri mazingira safi, manisipaa Ilala wametoa gari moja la takataka linazoa taka kila siku.
Kuhusu bidhaa katika soko hilo wanauza mazao ya samaki bidhaa zingine marufuku kuuzwa katika soko hilo.

Post a Comment