Ads

MBUNGE wa Viti Maalum (CCM)mkoa Kasikazini unguja atoa msaada UWT, asisitiza Umoja.


 NA Heri Shaaban,Unguja
Mwambawahabari
MBUNGE wa Vita Maalum (CCM)mkoa Kasikazini unguja  Angelina Malembeka  amekabidhi mashine tatu za kutengeza chaki kwa Wanawake wa Umoja wa  Wanawake (UWT) mkoa wa  Kaskazini Unguja  .


Mashine hizo za kisasa kwa ajili ya kutengeneza chaki zilikabidhiwa katika ziara endelevu ya Mbunge MALEMBEKA kukabidhi Katiba ya UWT na Kanuni zake mkoani Kaskazini Unguja.


Mbunge malembeka alitoa mashine hizo kwa Wanawake wa UWT Wilaya ya Kaskazini A ,UWT wilaya ya Kaskazini B na  Kikundi cha Ushirika kilichopo Mkoani humo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi mashine hizo katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha mapinduzi
aliwataka UWT washikamane wawe wa moja.

''Nimeanza ziara endelevu Mkoani Kaskazini Unguja katika utekelezaji Wangu wa Ilani kukamilisha vile nili vyoahidi  kama Mbunge wao kupitia viti maalum.

Aliwataka umoja wa wanawake kushikamana kuwa wamoja na UWT mpya  na kusimamia misingi ya Chama kwa kufuata kanuni.

Alisema atashirikiana UWT na kuwakikisha malengo ya UWT yanafanikiwa mkoa kaskazini unguja.

Akizungumzia msada wa mashine hizo za chaki alisema lengo la kuwapa mashine wazalishe chaki alafu wauze mashuleni kama sehemu ya mradi wao.

Alisema kuwa serikali inapotaka kuwagiza chaki wanatoa Mkoani Simiyu hivyo mradi huo mara baada kukamilika  chaki zitakuwa zinauzwa Mkoani humo.

"Natarajia kufanya ziara nyingine katika mkoa  huu kwa ajili ya utoaji wa Elimu ya mafunzo ya kutengezaji wa chaki Elimu hiyo itawasaidia wanawake wote wa UWT waweze kujua utengezaji wake" alisema.

Aidha alisema mara  baada kukamilika miradi itaongeza ajira kwa uwt  wote waliopo mkoa kaskazini unguja na aliwataka UWT Kitunza mashine hizo Mali yao wasije kuuza.


Alisema atashirikiana na serikali katika kukuza sekta ya elimu na kuwataka  UWT  wa mkoa kaskazini Unguja kupita katika mashule baade kutafuta soko la bidhaa hiyo  wasizubae katika kampeni ya Maendeleo Mkoa wangu kiwanda changu.


Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma alimponngeza Mbunge MALEMBEKA kwa hatua hiyo.

Waziri huyo wa Elimu alisema ameshukuru uzalishaji wa chaki ukianza halmashauri Zote zitachukua chaki katika mkoa wa Kaskazini Unguja. ..

No comments