Ads

WATANZANIA WATAKIWA KUSHIRIKI MAONESHO YA HUDUMA ZA AFYA MUHIMBILI

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel B. Aligaesha akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
MWAMBA WA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.

Watanzania wametakiwa kushiriki katika maonesho ya huduma za afya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili yanayotarajia kufanyika Juni I8 hadi 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel B. Aligaesha, amesema kuwa maonesho hayo yatafanyika kwa kipindi cha siku tatu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.

Aligaesha amesema kuwa lengo la  maonesho hayo ni kuwapa fursa wananchi kuona shughuli zinazofanywa na hospitali ya taifa ya muhimbili.

"Watanzania watapata elimu juu ya utaratibu wa kupata huduma, kutoa elimu ya afya kuhusiana na magonjwa mbalimbali pamoja na kutoa maoni na malalamiko juu ya huduma tunazotoa" amesema Aligaesha.

Amefafanua kuwa wataalam waliobobea kutoka maeneo mbalimbali ya hospitali  watakuwepo ikiwemo upande wa ushauri, uchambuzi, tiba na upasuaji, hivyo wanapaswa kujitokeza.
Kauli  mbiu ya maonesho ya mwaka huu ni Mapambano dhidi ya rushwa kwa kwa kushirikisha wadau na kujenga uongozi  bora ili kufikia malengo ya ajenda 2063 ya umoja wa Africa na malengo endelevu.

Maonesho hayo yameratibiwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ambapo yatafanyika kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa II jioni.

Hata hivyo imeelezwa kuwa maonesho ya huduma za afya hospitali ni sehemu ya matukio katika kalenda ya umoja wa afrika(AU) ambapo nchi wanachama huadhimisha kwa kufanya maonesho ya kazi mbalimbali zinazofanywa na serikali pamoja na taasisi zake.

Maonesho hayo yanaratibiwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambayo ufanyika kila mwaka kuanzia Juni I6 hadi 23 na mwaka huu mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.

No comments