WATOTO YATIMA NA WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU ZAIDI 220,WAPEWA TOTO AFYA KATI YA NHIF.
Na John Luhende
Mwambawahabari
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Makonda leo amekabidhi Kard za Bima ya Afya kwa Watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika Jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi Kadi hizo Makonda amesema kadi hizo zimefadhiliwa na Hospital ya Regency na TMJ za jijini Dar es Salaam na zitakuwa na uhai wa mwaka mmoja.
Pamoja na hayo Makonda amesema watoto wengine 400, watapatiwa msaada wa mabegi yenye vifaa vyote vya shule .
Kwaupande wake Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Daisy Majamba amesema Jumla ya Card 220 zimekabidhiwa, na kwamba kupatikana kwa watoto hao kulifanyika zoezi la kuwa tambua kutoka katika vituo mbalimbali vya kuelekea watoto jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Hospitali ya Regency Medical Center Dr Rajni Canabar amemshukuru mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Makonda kwa kuanzisha mchakato wa kumgawa Card hizo na wao kama wadau wamefurahi kushiriki katika kusaidia watoto hao na kuitaka jamii kuwa thamani na kuwa linda watoto hao na kuwa ona sawa na wengine.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi gharama matibabu ya Toto Afya Kadi ambazo ni kila moja ni shilingi 50400, kwa mwaka ni nafuu ukilinganisha na gharama za matibabu bila kadi hiyo.
Aidha ameitaka kutambua umuhimu wa Afya kwa Watoto wao kwa kuwa Katia Toto Afya Kard, na kuwataka wadau wengine kujitokeza kuzihuisha kadi hizo baada ya muda wake kwisha.
Post a Comment