DKT TIZEBA AZINDUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA YA KILIMO JIJINI DODOMA
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akizungumza wakati akifungua mkutano na kuzindua Baraza la wafanyakazi wa wizara ya kilimo kwenye ukumbi Wa Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) Mjini Dodoma, Leo 28 Juni 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba (Kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe (Katikati) na Katibu wa Baraza la wafanyakazi Wizara ya kilimo Bi Agnes Hugo wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa ufunguzi wa mkutano na uzinduzi wa Baraza la wafanyakazi wa wizara ya kilimo kwenye ukumbi Wa Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) Mjini Dodoma, Leo 28 Juni 2018.
Katibu Mkuu wa wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano na kuzindua Baraza la wafanyakazi wa wizara ya kilimo kwenye ukumbi Wa Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) Mjini Dodoma, Leo 28 Juni 2018.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano na kuzindua Baraza la wafanyakazi wa wizara ya kilimo kwenye ukumbi Wa Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) Mjini Dodoma, Leo 28 Juni 2018.
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano na kuzindua Baraza la wafanyakazi wa wizara ya kilimo kwenye ukumbi Wa Wakala Wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) Mjini Dodoma, Leo 28 Juni 2018.
Na Mathias Canal, WK-Dodoma
Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba leo 28 Juni 2018 amefungua
mkutano na kuzindua Baraza la wafanyakazi wa wizara ya kilimo, mkutano
utakaotuama kwa siku mbili kuanzia leo mpaka kesho 29 Juni 2018 katika ukumbi
wa Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) Jijini Dodoma.
Akizungumza katika mkutano huo Dkt Tizeba aliwasisitiza
wajumbe wa baraza hilo kwa umoja wao kujadili kwa muktadha wa kutatua
changamoto na kuboresha sekta ya kilimo kupitia mada mbalimbali
zitakazowasilishwa ikiwa ni pamoja na kuhusu elimu ya majukumu ya wajumbe wa
Baraza la wafanyakazi, Elimu juu ya watumishi wa Umma na hoja kutoka vyama vya
wafanyakazi sambamba na wajumbe kupitishwa katika bajeti ya wizara kwa mwaka
2018/2019.
Alisema kuwa Baraza la wafanyakazi ni chombo muhimu ambacho
kimepewa nguvu kisheria ili kuwapa watumishi nafasi ya kushiriki katika maamuzi
ya utekelezaji wa masuala mbalimbali yanayohusu utendaji na ufanisi wa Taasisi
ili kuongeza tija mahali pa kazi hivyo wajumbe hao wanapaswa kujadili mada hizo
kwa ufanisi na tija.
Alisisitiza kuwa Baraza hilo linapaswa kuzaa matokeo mazuri
ikiwemo uboreshaji wa mazingira ya kazi huku akisema kuwa serikali imekuwa
ikisisitiza kila taasisi ya umma kuunda mabaraza ya wafanyakazi ili kuongeza
ufanisi na tija katika mchango wa mapinduzi ya uchumi wa viwanda.
Alisema, serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli inatambua
ushirikiano wa pande hizo mbili katika maamuzi hivyo ni vigumu kutekeleza
majukumu endapo pande moja haitashirikishwa kwani umuhimu huo umetiliwa mkazo
na kupitia sera, sheria na kanuni zinazosimamia uendeshaji wa taasisi za umma.
Katika hatua nyingine Mhe tizeba aliwakumbusha wajumbe hao
kuwa miongoni mwa majukumu muhimu ya sekta ya kilimo ni pamoja na kutambua kuwa
katika maendeleo ya nchi asilimi 66.5 ya watanzania wanategemea sekta ya kilimo
pamoja na kuhakikisha usalama wa chakula nchini hivyo ni vyema katika mkutano
huo kujadili mada hizo na kuwa na mategemeo ya kuwanufaisha zaidi wakulima kote
nchini.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi
Mathew Mtigumwe akizungumza kabla ya kumkaribisha waziri wa kalimo kufungua
kikao hicho cha Baraza la wafanyakazi alisema kuwa Baraza hilo jipya limeundwa
kufuatia Baraza la awali kufikia muda wa ukomo wake baada ya maridhiano baina
ya Menejimenti ya wizara ya kilimo na vyama vya wafanyakazi vya TUGHE na RAAWU
kufikiwa.
Mhandisi Mtigumwe aliongeza kuwa Mkutano wa Baraza la
wafanyakazi ni sehemu ya utekelezaji wa sheria ya ajira na mahusiano kazini Na
6 ya mwaka 2004 na sheria ya majadiliano ya pamoja katika utumishi wa umma Na
19 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2005. Ambapo kwa mujibu wa sheria hizo
lengo la kuanzishwa mabaraza ya wafanyakazi ni kuwa na chombo cha ushauri na
majadiliano ya pamoja kati ya wafanyakazi na waajiri ili kuwa na ushirikishwaji
mpana wa wafanyakazi mahala pa kazi.
Alisema, kufuatia mabadiliko ya muundo wa Wizara ya kilimo
hususani baada ya idara ya utafiti kuwa Taasisi inayojitegemea imelazimu muundo
wa Baraza hilo kufanyiwa mabadiliko na kupelekea kupungua kwa idadi ya wajumbe
kutoka 98 hadi kufikia 57, Aidha, mkataba mpya wa kuunda Baraza la wafanyakazi
umezingatia mabadiliko hayo.
MWISHO.
Post a Comment