CROATIA YAMFUKUZA MSHAMBULIAJI WAKE KOMBE LA DUNIA
Mshambuliaji wa Croatia Nikola Kalinic amefukuzwa kutoka mechi ya kombe la Dunia nchini Urusi baada ya kukataa kuingia uwanjani wakati mabadiliko ambapo Croatia ilishinda Nigeria 2-0.
Nafasi ya mchezaji huyo wa miaka 30 haitachukuliwa na mtu mwingine ikimaanisha kuwa kikosi kitabaki na wachezaji 22 kwenye Kombe la Dunia.
Kalinic, mchezaji wa AC Milan anasema ana jereha la mgongo baada ya kulalamikia tatizo hilo wakati wa mechi ya kirafiki na Brazil.
Kocha Zlatko Dalic alisema: "Ninataka wachezaji wangu wawe sawa na tayari kucheza."
Kalinic ambaye aliichezea Blackburn Rovers kati ya mwaka 2009 na 2011 amefunga mabao 15 kwa mwezi 41 kwa Croata.
- Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 19.06.2018
- Wachezaji wa Saudi Arabia wanusurika na ajali ya ndege Urusi
"Wakati wa mechi na Nigeria, Kalinic alikuwa akifanya mazoezi na alistahili kucheza kipndi cha pili," Dalic alisema.
Lakini akasema kuwa hakua tayari kutokana na matatizo ya mgongo.
Croatia watacheza na Argentina siku ya Alhamisi na kumalizia kundi lao la D dhidi ya Iceland Jumanne tarehe 26.
Wachezaji wengine watano waliohama Kombe la Dunia mapema
Willie Johnston (Scotland)
Mchezaji huyo wa West Brom alifukuzwa kutoka Kombe la Dunia 1978 huko Argentina na shirikisho la kandanda la Scotland baada ya kupatikana kutumia madawa ya kuongeza nguvu za mwili.
Roy Keane (Jamhuri ya Ireland)
Kuondoka kwa kiungo huyo wa kati wa Manchester United kutoka kambi ya mazoezo ya Jamhuri ya Ireland ilikuwa moja nyakati zinazokumbukwa sana wakati wa Kombe la Dunia la mwaka 2002.
Hakufurahishwa na jinsi Ireland ilifanya maandalizi yake hali iliyosababisha kuwepo majibizano na kocha Mick McCarthy mbele ya wachezaji wengine.
Licha ya kujiandaa kucheza mechi ya ufunguzi na Cameroon, Keane alibaki akitembea na mbwa wake kwenye mitaa ya Cheshire.
Diego Maradona (Argentina)
Nyota huyo wa Argentina alitimuliwa kutoka kwa kombe la dunia la mwaka 1994 lililoandaliwa nchini Marekani kabla ya mechi ya mwisho ya makundi na Bulgaria.
Alikuwa awali ameiongoza Argentina kwenda kombe la Dunia la mwaka 1986 na 1990 ampapo walipoteza dhidi ya Ujerumani.
Maradona alifunga wakati wa ushindi wa mabao 4-0 kabla ya kupatikana kutumia madawa ya kuongeza nguvu za mwili na kufikisha kikomo taaluma yake.
Nicolas Anelka (Ufaransa)
Mshambuliaji huyo wa Ufaransa aliondolea kutoka kikosi cha nchi yake nchini Afrika Kusini baada ya kutofautiana na kocha.
Mshambuliaji huyo ambaye wakati huo alikuwa akiichezea Chelsea alimshambulia kwa maneno meneja wakai wa kipindi cha mapumziko wakati wa mechi ya kombe la duni na Mexico mwaka 2010 waliposhindwa na Mexico mbaao 2-0.
Alikataa kuomba msamaha na licha ya wachezaji wengine kulamika jinsi alitendwa aliamrishwa kurudi nyumbani na sihrikisho la kandanda la Ufaransa na kupigwa marufuku ya mechi 18.
Zlatko Zahovic (Slovenia)
Roy Keane hakuwa mchezaji pekee kuondoka Kombe la Dunai la mwaka 2002 baada ya mchezaji wa Slovenia Zahovic kumfuata nyuma.
Kioungo huyo wa wakati wa Benfica alikuwa na tofauti na kocha Srecko Katanec baada ya kumuondoa uwanjani wakati wa mechi waliyoshindwa na Spain 3-1 ambapo shirikisho la kandanda kuamua kumtimua mapema. Kutoka bbcswahili.
Post a Comment