ASILIMIA 7 HADI 16 YA WANAWAKE WOTE DUNIANI NI WAJANE
Mwamba wa habari
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa unaonesha kuwa kati ya asilimia 7 na 16 ya wanawake wote duniani ni Wajane.
Jamii
imetakiwa kuendeleza mipango na kuongeza juhudi zaidi katika
kukabiliana na vitendo vya ukatili, unyanyasaji na kuwainua wajane ili
wapate uwezo wa kiuchumi wa kuzihudumia familia na wategemezi wao kwa
kuwa ndiyo muhimili pekee wa familia iliyoachwa.
Akiongea
kwa niaba ya Mgeni rasmi wa kongamano la Wajane liliofanyika leo katika
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa Bi.
Honoratha Rwegasira amepongeza juhudi za wadau wa maendeleo na serikali
katika kuwasaidia wajane kuleta usawa wa kinjisia na kuinua ushiriki wao
katika ngazi za kutoa maamuzi.
Aidha
Bi.Rwegasira ameitaka jamii kuacha mila potofu kama vile kunyanganya
mali mjane, kuozesha watoto wa kike katika umri mdogo, kurithi wajane na
nyingine zote zinazoweza kumdhoofisha mwanamke katika jitihada zake za
kujikwamua kifikra, kiutamaduni, kiuchumi,kijamii na kisiasa.
Wakati huohuo Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia kutoka Wizara ya
Afya,Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Mwajuma Magwiza amesema kimsingi
lengo la maadhimisho ya Siku ya Wajane Duniani ni kutoa nafasi kwa Wadau
kushirikiana na Serikali kwa kutoa huduma za msingi kwa wajane na
kuondoa aina zote za ukandamizaji ikiwemo haki ya kumiliki mali,
umasikini, mira na desturi za kurithiwa baada ya kufiwa.
Aidha
Bi. Magwiza ametaja mipango ya baadae ya maadhimisho haya kuwa ni
kuhakikisha wajane wanapata haki za msingi,kuainisha maeneo na takwimu
za mila na desturi kinzani na haki za wajane mengineyo ni kushawishi
wadau kuchangia katika uwezashaji wanawakwe kiuchumi hasa kundi la
wajane ili kuondokane na umasikini wa kaya.
Kongamono
hilo pamoja na kuwakutanisha Wajane wa Jiji la Dodoma pia
limewakutanisha wadau wa masuala ya haki za wajane ambapo Mwakilishi
kutoka shirika la TAWIA Bi.Neema Duma ameitaka serikali kuhakikisha
wajane wanapewa hati za vifo vya waume zao pia kutaka masuala ya wajane
yanashughulikiwa kimkakati zaidi na kuunda mfuko wa wajane wenye umri
mkubwa na wale wasiojiweza kabisa.
Tarehe 23, Juni kila mwaka ni
Siku ya Wajane Duniani ambayo chimbuko lake linatokana na mwanaharakati
Pushpa Vati Loomba ambaye alishuhudia mama yake akikabiliwa na shida
nyingi baada ya kufiwa na mme wake Juni 23, 1954 na kuanzisha Loomba
Foundation kwa ajili ya kampeini ya kueleza shida za wajane ambazo
hazionekani, zimesahaulika na hazisemwi popote.
Post a Comment