KILA MCHUMA JANGA HULA NA WAKWAO , TUNISIA HATUNAO TENA KOMBE LA DUNIA.
Mwamba wa habri
Tunisia
imepokea msiba mwingine katika michuano ya Kombe la Dunia baada ya
kukumbana na kipigo cha mbwa koko cha mabao 5-2 kutoka kwa Ubelgiji.
Katika
mchezo huo wa Kundi G uliopigwa Uwanja wa Spartak, Ubelgiji wamejipatia
mabao yao kupitia kwa Romelu Lukaku aliyefunga mawili.
Mabao
mengine ya Ubelgiji yaliwekwa kimiani na Eden Hazard aliyefunga mawili
pia moja likiwa la penati, pamoja na Michy Batshuayi katika dakika ya
90.
Mabao ya Tunisia yaliwekwa kimiani na Dylan Bronn katika dakika ya 18 ya kipindi cha kwanza na Khaziri dakika ya 90+3.
Msimamo
wa kundi hilo unaonesha Ubelgiji ipo kileleni ikiwa na alama 6 kisha
ikifuatiwa na England yenye 3 huku Panama na Tunisia zikiwa hazijapata
alama yoyote.
Post a Comment