WANAO CHEZESHA MAMLUKI MASHINDANO UMISETA WAPEWA ONYO
Mwamba wa habari
MAOFISA Elimu Sekondari wa manispaa tano mkoani Dar es Salaam ambao wanafunzi wao wanashiriki Mashindano ya Umoja wa Shule za Sekondari (UMISSETA) wameshauliwa katika mashindano hayo wasiweke wachezaji mamruki.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana katika ufunguzi wa Mashindano ya UMISSETA Mkoa Dar es Salaam na Ofisa Elimu wa Mkoa huo Khamis Lissu.
Lissu alisema katika mkoa wake wachezaji 750 wameshiriki mashindano hayo ya mkoa inatafutwa timu moja itakayoshiriki mashindano ya ngazi ya UMISSETA Taifa.
"Kila mwaka mkoa wangu wa Dar es Salaam unafanya vizuri mwaka jana tunachukua kombe ngazi ya Taifa Mwanza na Mwaka huu tutafanya vizuri tutaleta vikombe vyote"alisema Lissu.
Aliwataka maofisa elimu wake wa ngazi za manispaa katika kufanya usaili waweke wachezaji ambao wana sifa na wasiopitiliza umri ili wasitie doa katika mashindano ya ngazi ya TAIFA.
Alisema mwaka huu wachezaji wake wapo vizuri katika kambi Jitegemee wanamichezo 750 wakiwemo wanafunzi 650 na walimu, makocha na viongozi 100.
"Wakurugenzi wa manispaa zote wamejitahidi na wameakikisha wilaya zao zinakuwa na timu bora ambazo kwa pamoja zinashindana katika michezo mbalimbali ili kuweza kupata wachezaji wa mkoa na wachezaji mahiri"alisema
Aidha alisema kwa mwaka 2018 michezo inayoshindaniwa ni, mpira wa Wavulana na wasichana, netiboli kwa wasichana,mpira wa mikono kwa wasichana na Wavulana, mpira wa wavu kwa Wasichana na Wavulana,mpira kikapu kwa wasichana na wavulana, riadhaa kwa wanafunzi wa kawaida na wenye mahitaji Maalum,Tenis,Bao,na fani za ndani, pamoja na ngoma, kwaya, ngonjera na Mashairi.
Alisema mkoa wa Dar es Salaam mwaka 2017ulikuwa Bingwa wa umisseta Kitaifa kwa kushinda mikoa yote iliyoshiriki mashindano hayo na mwaka huu mkoa Dar es Salaam umejipanga kufanya vizuri zaidi kuchukua vikombe vingi kwa mshindi wa kwanza kama ilivyokuwa mwaka 2017.
Lissu alisema kupitia michezo hiyo watapatikana wanamichezo bora zaidi ambao watapambana kuhakikisha ushindi haupotei kwani dhamira wanayo, Nguvu wanayo na uwezo wa kutosha pia wanao
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dar Es Salaam Jumaane Ndayigeze alisema Ofisi ya Rais TAMISEMI imetoa mwongozo wa uendeshaji michezo hii ya umisseta ambapo michezo uanzia katika ngazi ya shule, kata Klasta, Wilaya, mkoa na hatimaye TAIFA.
Post a Comment