WANAWAKE ILALA WASHIRIKISHA WASICHANA KASULU KUPANDA MITI.
Mwamba wa habari
Katika kuazdhimisha siku ya mazingira Dunani Wanawake wa Manispaa ya Ilala, leo wameendesha zoezi la kupanda Miti katika Shule ya Secondary Kasulu iliyopo maeneo ya Ilala ambapo wanafunzi wa shule hiyo wameshirikishwa kikamilifu katika zoezi hilo.
Akizungumza katika zoezi hilo Afisa mazingira wa Manispaa ya Ilala Feada Magesa amesema wameamua kuwashirikisha wasicha katika upandaji miti ili kuwajengea moyo wa kupenda Mazingira ilikuweza kushiriki katika kutunza mazingira kupambana na hewa ya Ukaa katika maeneo yao watakapokuwa wamepanda miti.
‘’Hiisiku tumeitenga sisi wanawake wa Ilala ili kuweza kupandikiza moyo watoto wa kike wa sekondari na shule za Msingi kupanda miti katika mazingira yao’’ Alisema.
Aidha amesema baada ya kutembelea shule mbali mbali katika Manispaa ameona shule hiyo ni mpya na haina miti hivyo kwa leo wamepanda miti 110 katika maeneo ya shule hiyo na amewasisitiza wanafunzi kuitunza miti hiyo iweze kukua ili kuhifadhi mazingira ya eneo hilo, na amewashukuru walimu na wanafunzi kuwapokea vizuri .
‘’ kwakweli wametupokea vizuri kamaulivyo ona wasichana wamefurahia sana kushiriki zoezi hili nao wamepanda miti naiman wataituza kwa kuimwagilia maji hadi itakapokua’’.Alisema Magesa .
Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule hiyo Christina Kaswaga ,ameshukuru idara ya Mazingira kwa kuichagua shule hiyo kupanda miti katika maeneo hayo kwani shule zikonyigi na kushikisha wasicha kaika zoezi hili kumeleta changamoto kuona kuwa nao wanweza kushiriki uhifadhi wa mazingira , na ameahidi kuendelea kusimamia kuitunza miti hiyo na mazingira ya shule hiyo.
Kwa upane wao wanafunzin wakike walishirikia zoezi hilo wameshukuru uongozi wa Mazingira Ilala kuwafikia katika shule yao kwani baadhi yao kutokanana mazingira wanayo toka hawana maeneo ya kupanda miti na hawajawahi hatata kupanda miti hivyo leo imekuwa siku muhimu sana ambapo wamejifunza na kupanda miti .
‘’Naitwa Rehema Shabani mimi nilikuwa sija wahi kupanda miti hata siku moja nimependezewa sana na upandaji miti name kwa mara yangu ya kwa nza nimepanda mti, ntahakikisha mti wangu nautuza hadi uwe mti mkuwa na utakuwa wa ukumbusho’’.Alisema
Siku ya mazingira Duniana huadhimishwa kila mwaka ambapo mwaka huu itaadhimishwa tarehe 5 Juni ,na kaulimbiu itakuwa ‘’Mkaa ni gharama tutumie Nishati mbadala’’.
Post a Comment